Promote your business for free grow your business for life you don't need to spend more money anywhere.

THIS BLOG IS SPONSORED BY AHADIWAY ,ADVANTAGES FOR JOINING AHADIWAY BOON CAREER (ABC) CHAPTER = Employment opportunities within and outside the country. , Job experience , Self -employment , Field stations, part time jobs and chances to be trained.

Thursday, May 17, 2012

wewe upo kundi gani kati ya hao

Wanawake wengi sasa hivi wanajikuta kwenye mapenzi kwa mkumbo kwamba wanataka tu waonekane wako kwenye uhusiano, wengine wanatafuta kitu gizani kwa kupapasa wakipata wanatulia, wengine wanazunguka na watu weengi wakidhani ndio namna yakuondokana na a broken heart, wengine walioko kwenye mapenzi wanaruka kamba migongoni kwa wanaume zao ili wakilalamika tu wao washuke na kuondoka zao, wengine huwafunga wanaume zao midomo kwa kuwatishia kuwaacha-hawa wako wengi sana, wengine hutengeneza mapenzi ili kumvuta wampendaye, wengine hutumia mavazi wakidhani yanaweza kuchukua nafasi ya moyo au utu, wengine hudiriki kuwakimbia waume zao ili eti wapime upendo wa waume zao kwao-(hii huwaumiza wanaume wengi moyoni na wala haiongezi mapenzi inazidisha mashaka), wengine huchukia mapenzi ya kweli nakuona kama yanaleta usumbufu, wengine hujali zaidi watu wengine kuliko waume zao, wengine husahau kama ndoa ni jukumu na kuishia kuikwepa kwa kufikiria jukumu hilo ni lamwanaume pekee, wengine hudiriki kuacha kunyonyesha watoto wao wenyewe kwa kudhani wataharibu maumbo ya matiti yao, wengine hudhani kufanya mapenzi ndio njia ya kumridhisha mwanaume, wengine hudhani mwanaume wake asipomtafuta basi yuko na mwanamke mwingine, wengine huchelewa kupokea simu zao kwa kudhani kwa kufanya hivyo wataleta hamasa ya penzi toka kwa mwanaume-kiukweli hii hukasirisha tu, wengine hufikiri kupika na usafi wa nyumba ni kazi ya housegirl na kuangalia homework ya mtoto ni kazi ya mwalimu, wengine huchukia watoto wao wenyewe na kudiriki hata kuwatupa angali wachanga, wengine hudhani kusoma ni jukumu la mwanaume kwasababu wao wataolewa, wengine hudhani kutumia zaidi kwenye starehe ndio njia yakuonekana unamaendeleo, wengine humsahau Mungu na kujikuta wakimkumbuka tu wakiwa na matatizo au zikifka sikukuu za kidini, wengine hudhani unene ni afya, wanawake wengine hudhani kulia ndio namna pekee yakujijengea mazingira ya kusamehewa wafanyapo kosa, wanawake wengine huiba kwa wanawake wenzao

No comments:

Umesoma hizi hapa