============
MODERATOR:

Tunajaribu kupata usahihi wa habari hii, ikibainika mwanzishaji hoja kadanganya atachukuliwa hatua stahiki na ikiwa kuna ukweli basi hoja itaruhusiwa kwa mjadala zaidi.

============


Taarifa iliyotufikia hivi punde...

Mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na aliyekuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi wa Richmond Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa amezidiwa na kuanguka akiwa nyumbani kwake Jijini Dar es salaam.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, Mheshimiwa Lowassa ameamka leo asubuhi akiwa hajisikii vizuri na alishindwa kufanya mazoezi ya asubuhi kama ilivyo kawaida yake. 

Majira ya saa tatu asubuhi, Mhe. Lowassa akiwa anajiandaa kupata kifungua kinywa alianguka ghafla ukumbini kwake na kupoteza fahamu. Mlinzi wake Bw. Tendewa na wasaidizi wake walihaha kumuita daktari aje kumchunguza na kumtibu. 

Mtoto wa Mgombea huyo wa UKAWA, familia na baadhi ya viongozi wakuu waChadema wapo kwenye sintofahamu kubwa na wamekubaliana kutosema chochote, na kwamba Viongozi hao wa Chadema wamepanga kufanya kikao leo jioni kujadili tukio hilo na hatma ya shughuli ya ufunguzi wa Kampeni kesho kutwa tarehe 22.

Kwa miaka kadhaa sasa, afya ya Mheshimiwa Lowassa imekuwa ni gumzo kubwa kutokana na muonekano wake kudhihirisha kwamba ana tatizo kubwa la kiafya. Mara kadhaa amelazimika kujitetea au kuizungumzia afya yake. 

Katika ziara yake ya mikoani baada ya kujiunga na Chadema, wananchi wengi wamekuwa wanajitokeza kumpokea. Hata hivyo, baada ya mikutano hiyo, wananchi wamekuwa wanarejea majumbani wakiwa na minong'ono ya kukata tamaa baada ya kuishuhudia hali ya afya ya Lowassa. Katika hotuba zake mikoani, wananchi wamekuwa wanapata tabu kumsikia anasema nini na amekuwa anazungumza kwa muda mfupi sana. Kwa mfano, alipohutubia Arusha, alizungumza kwa dakika nne tu. 

Kabla hajaamua kugombea Urais hata ndani ya CCM, kulitokoea mjadala mkubwa ndani ya familia na baadaye mgawanyiko mkubwa kuhusu haja na ulazima wa yeye kugombea kutokana na afya yake kuzorota. Watoto wake wawili wadogo, akiwemo Robert au maarufu kama Bob, walitaka baba yao apumzike siasa na ajitazame afya yake. Lakini watoto wake wawili wakubwa, Pamela na Cadet (Freddy) wao walimhimiza agombee. 

Mgombea huyo wa UKAWA ametumia juhudi kubwa sana kuficha utata wa afya yake. Kwa mfano, wakati anatafuta wadhamini katika mchakato wa CCM,alizunguka nchi nzima kwa ndege na kwa helikopta. 

Hata hivyo, hakuna pahala popote ambapo unaweza kuona picha ya hiyo ndege wala helikopta. Picha zote zinaonekana yuko kwenye gari au anahutubia. Hii inatokana na ukweli kwamba amefanikiwa kuwaweka mfukoni waandishi karibu wote hapa nchini ambao wameamua kuazima akili zao kutoka kwa Bwana Kibanda ambaye huwaamulia nini waandike.