Promote your business for free grow your business for life you don't need to spend more money anywhere.

THIS BLOG IS SPONSORED BY AHADIWAY ,ADVANTAGES FOR JOINING AHADIWAY BOON CAREER (ABC) CHAPTER = Employment opportunities within and outside the country. , Job experience , Self -employment , Field stations, part time jobs and chances to be trained.

Tuesday, November 23, 2010

wanaume bwana!!!! makubwaMISS. Dona Stephen

Nianze kwa kuongea na wanawake. Kimaumbile wanaume wanapenda kuona wanasikilizwa na wake zao na hawakawii ‘kukubadilikia’ unapowakwaza. Pamoja na kwamba nanyi mna sauti ndio, lakini wanaume ni watu wa kuwasoma kwanza na kuwaendea taratibu kuliko kuwapandishia na kuonesha kushindikana nao. Kama kweli unampenda basi muoneshe unamheshimu, hapo utampata!Wanaume hupenda wanawake wasafi, wakarimu, wacheshi na wasio na kiburi wala ‘nongwa’ zisizokuwa na maana, jitahidi katika hayo ili ukonge moyo wa mpenzi wako na kamwe hatakusaliti.

Lakini huwa nasikitishwa sana na hizi zama za usawa ambazo zinachochea migogoro mingi katika ndoa. Kwa mfano, hivi sasa mwanamke kumtii mumewe kunachukuliwa ni kama utumwa!


Nawahakikishia, kwa ninavyofahamu hisia za wanaume walio wengi, hali hii ikiendelea sidhani kama kutakuja kuwa na mapenzi imara, sana sana mapenzi yatageuka kuwa uwanja wa mapambano na ushindani siku zote.


Nawaomba wanawake, pamoja na elimu mliyonayo na visomo vya hali ya juu, jitahidini kujilazimisha kuwaheshimmu waume zenu kwani kamwe hamtapungukiwa na kitu bali mtajihakikishia mapenzi yenye utulivu na amani siku zote za maisha yenu!


Nikiwageukia wanaume, akina kaka na akina baba, ninyi mnachukua nafasi ya baba yenu Adamu. Baba yetu Adamu alimpenda mke wake kwa dhati hata akashawishika kula tunda alilokatazwa ili mradi asimsononeshe mkewe.


Yawapasa mfahamu kuwa wanawake ni zawadi kwenu, pumziko na tulizo la mioyo yenu. Wanawake ndio raha yenu na amani kubwa ya maisha yenu.Kosa kubwa mnalofanya wanaume ni kuutumia vibaya “mfumo dume” hasa katika suala nyeti kama mapenzi. Mapenzi si ubabe, mapenzi ni upole na ukarimu. Pamoja na kwamba mmebarikiwa kwa kupewa nafasi ya kuwa ‘kichwa katika nyumba’ lakini linapokuja suala la kurekebisha tofauti zinazojitokeza katika uhusiano wenu, si vyema kutumia njia za kibabe.


Niwaambie kitu, wanawake ni wa ‘hisia’ zaidi na waliobarikiwa upendo wa hali ya juu na ndio maana wakapewa dhamana ya kubeba mtoto tumboni kwa miezi tisa na pia kumnyonyesha na kumlea kwa miaka kadhaa, wewe ungeweza?
Nasema ni watu wa hisia kwa sababu, hivi uliwahi kufikiri ni kwanini wanawake huridhika sana na kujisikia poa kweli wanapopewa zawadi kama ya maua na kadi zenye ujumbe wa mapenzi ukilinganisha na wanaume? Unafikiri ni kwanini wana machozi ya haraka wanapotendwa? Au unafikiri ni kwanini wanapenda kutumiwa meseji za kimahaba ‘love message’ zaidi kuliko kupigiwa simu? Jiulize.


Mimi nawaona wanawake kama watu wa kuheshimiwa na kupendwa sana. Mkumbuke wanawake ndio mama zetu, walezi wetu na ndio nyumba zetu. Ridhika na mpenzi uliye naye, heshimu hisia zake na thamini mapenzi yake kwako na mpe ile kitu roho inapenda!

5 comments:

Anonymous said...

very well said....the society needs to adapt this.

Tutafika said...

nimeipenda hii

Anonymous said...

Hiyo ni kweli dada.

Anonymous said...

ukweli ni kwamba katika kupeana haki au usawa inatakiwa heshima uwepo kati ya mwanaume na mwanamke sivyo hakuna ndoa . hivyo basi kwa mwenendo huu tutegemee kuwa usawa wa mwamnaume na mwanamke utakuwepo bila ndoa . kwani toka Mwanzo Mungu aliumba mwanaumme na mwanamke katika usawa lakini bado waliheshimiana na kuthaminiana na ndoa iliendelea kama kawaida. lakini hii ya leo wengi wanadhana usawa ni kila mtu kufanya ya kwake mwenyewe bila mpenzi wake kujua na pia wanadhani kuwa usawa ni kuacha majukumu yao. kwa mfano mwanamke anatakiwa ajue mpaka wake katika usawa huo na majukumu yake katika familia.hivyo hivyo na mwanaume ajue majukukumu na mipaka yake kama baba wa nyumbani kama Mungu alivyoweka mipaka hiyo tangu mwanzo.Mwanamke anatakiwa kuwa hata awe na cheo kikubwa cha namna gani lakini kwa mume wako anatakiwa abaki na heshima kama mke, mwanaume naye afuate nyayo hiyohiyo ya kutambua mipaka yake kwa kumthamini na kumpenda mke wake.lakini bila hivyo tujiandae kuishi bila mwanaume au mwanamke huko mbele tunakoenda na hapo ndipo tutashuhudia jamii ya ajabu haijawahi kutokea duniani.
By.raphfokello@yahoo.com

Mickael mboya said...

nice thought presentation mummy just adding to wat u were sayn it is beta that women dont confuse haki sawa kwa wote/ haki za wanawake with power struggles

men r fighters by nature n hate loosing u can see it even from wild animals, nature has given women power of care love patience n forgiveness use this power to ur advantage .... if u respect ur man enough ur suggestion counts more than u think as far as we dont think its a show off that u can or a competition it always count.

Umesoma hizi hapa