Promote your business for free grow your business for life you don't need to spend more money anywhere.

THIS BLOG IS SPONSORED BY AHADIWAY ,ADVANTAGES FOR JOINING AHADIWAY BOON CAREER (ABC) CHAPTER = Employment opportunities within and outside the country. , Job experience , Self -employment , Field stations, part time jobs and chances to be trained.

Thursday, May 2, 2013

HISTORIA YA WAPARE

Wapare ni kabila kutoka milima ya Pare, Mkoa wa Kilimanjaro, kaskazini mwa nchi ya Tanzania. Lugha yao ni Kipare (au Chasu).

Wapare wanatokea katika wilaya za Same na Mwanga, mkoa wa Kilimanjaro, lakini pia wapo katika wilaya ya Moshi sehemu za Chekereni, Himo, Mabungo,Uchira, Moshi mjini, na pia katika wilaya ya Hai sehemu za Rundugai na mto Weruweru. Wapare pia wanaishi katika wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, sehemu za Bumbuli na Mavumo.Lakini kutokana na mahusiano yaliyopanuka hapa nchini,Afrika na dunia nzima kwa ujumla kutokana na suala la utandawazi wapare wametapakaa kote Tanzania kwa shughuli mbalimbali kwa mfano jamii kubwa ya wapare waliohamia mkoa wa Morogoro na kujenga makazi na hali imekuwa katika mikoa yote hapa nchini na kwingineko. Wapare wanasemekana wametoka katika nchi ya Kenya sehemu za Taita, Taveta na Ukamba. Ni kabila la watu wachache lakini wana ushawishi mkubwa katika nyanja za siasa na uchumi wa Tanzania. Wapare ni miongoni mwa makabila ambayo watu wake wamesoma sana. Wapare pia ni kabila la watu wanaopenda haki (yaani hawapendi kuonewa wala kumuonea mtu).Ndio maana watu wengine wanadhani wanapenda kesi,bali kesi ni njia mojawapo ya kuhakikisha haki inatendeka katika jamii.Utawasikia watu wengine wakidai kuwa mpare yupo tayari kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku. Dhuluma kwa Wapare ni kitu kilichokuwa kimepigwa marufuku hata kwenye matambiko yao, japo siku hizi kuna uwezekano baadhi yao wakawa hawana sifa hii tena.
Wapare walianza kufua chuma kabla ya mwaka 1700 na wafuaji walikuwa wakiitwa Washana, na huo ukoo upo hata leo hii. Wapare walikuwa wakiuza bidhaa zinazotengenezwa na chuma kama majembe,mapanga, visu, silaha kama mikuki kwa makabila ya jirani mfano Wachaga,na wamekuwa na uhusiano tangu siku nyingi. Bidhaa zao hizi ziliuzwa hata kwa Wasambaa (Washambaa).
Jamii za Wapare zimegawanyika katika makundi ya Wafugaji na Wakulima. Wakati Wafugaji wengi walihamia katika tambarare za Upareni, Wakulima wao waliishi milimani na wafuaji wa vyuma walikaa maeneo yote yaliyokuwa na uwezekano wa kupata chuma. Kwa asili Wapare hupeleka vijana wakiume jando (mshitu) ambako walipata mafunzo jinsi ya kuishi na familia,japo siku hizi tamaduni za kupeleka vijana mshitu hufanywa na watu wachache. Hata hivyo wapare wa Mwanga wamegawanyika katika jamii mbili: Wasangi na Wagweno. Wakati wasangi wanaongea kipare kinachoongelewa pia na Wapare wa maeneo mengine, Wagweno wao wana lugha yao iitwayo Kigweno. Kigweno ni mchanganyika wa Kipare na Kichagga. Hii inaonesha kuwa asili ya Wagweno ni uchagani japo zipo nadharia kadha wa kadha zinazoeleza asili ya wagweno kuwa huenda hata hawana asili ya uchaga wala upare lakini mbali na uhusiano wa lugha kinachofanya waonekane kuwa ni sehemu ya wapare ni namna tamaduni zao nyingine zinavyofanana na wapare,pia kuchanganyika katika maisha ya kila siku kwenye milima ya wapare pamoja na wagweno wengine kuwa na majina ya koo zinazofanana na za wapare kama Wasuya na Wavungi. Hata hivyo mila na desturi nyingi za Wagweno zinafanana zaidi na zile za wapare wengine.
Wapare ni wachapakazi sana wakichanganya kilimo, ufugaji na biashara, ndio maana hata leo wana uchumi mzuri katika viwango vya Tanzania. Zamani Wapare walikuwa na sala tofauti,kwa kila koo na eneo lao la tambiko, katika karne ya 19 hadi 20 wamisionari waliingia maeneo mengi ya Upare.
Imani za Wapare kwa sasa zinatofautiana kutokana na maeneo, walio Kusini mwa wilaya ya Same katika maeneo ya Ndungu,Kihurio,Bendera,Hedaru, Makanya,Suji,Chome,Tae,Gonja, Mamba hadi Vunta kuna waumini wa kanisa la Sabato wengi sana,maeneo kama Chome,Mbaga,Gonja, Vudee yana waumini wengi wa kanisaa la Kilutheri, Katika Wilaya ya Mwanga kuna idadi kubwa ya Walutheri na Waislamu. Wakatoliki, japo ni wachache, wanapatikana zaidi katika maeneo ya Kisangara juu, Vumari, na Mbaga.
Wapare pia wana ukaribu na makabila ya Mkoa wa Tanga hasa Wasambaa, Wazigua na Wanguu. Ukaribu wao uko katika lugha ambapo maneno mengi ya makabila haya yanafanana. Vile vile hata majina ya baadhi ya maeneo yaliyopo kwa Wapare yapo pia kwenye maeneo wanamoishi makabila kama vile Wasambaa na Wanguu. Kwa mfano, kwa Wapare kuna majina ya maeneo kama vile Gonja, Ndeme, Ndolwa n.k. Majina haya yapo pia maeneo ya Wanguu na Wasambaa. Hii inaonesha kwamba makabila haya yana asili moja.
Kuna watu wanadai kwamba Wapare asili yao ni uchagani. Eti Wapare kwa Kichagga mana yake ni "wapige". Hii si kweli kabisa. Isipokuwa watu wa makabila haya wote walitokea Kenya. Wachagga walitangulia wakawahi kuishi maeneo yenye rutuba hasa kuzunguka mlima Kilimanjaro. Wapare walikuja baadae na walipotaka kuishi na wachagga ndipo vita ikatokea kati ya Wapare na Wachagga. Ili kuepusha umwagaji damu zaidi Wapare walisogea kusini zaidi kuelekea mkoa wa Tanga. Wapare wenyewe kwa asili hujiita Vaasu ikiwa na maana ya "vareasa" au watu wanaotumia mishale
Wapare wana koo nyingi na majina mengi yakiwa na maana ya maeneo ya asili yao au mazingira ya kuzaliwa kwao,mfano Mbwambo,Mjema,Msangi,Mgweno,Mvungi,Msuya,Mgonja n.k, wana asili ya maeneo yao.
Mifano ya majina ya watoto wa kipare
Majina ya kike: (Mazina a vabora va Chasu)
Ingiahedi, Itikija, Kafue,Kapingu, Kapwete, Kodawa, Kokiambo, Komkwavi, Kompeho, Kondisha,Ludao, Mchikirwa, Mshinwa, Naanjela, Nacharo, Naelijwa, Naetwe, Nafue, Nahuja, Nakadori, Nakiete, Nakijwa, Nakimo, Nakunda, Nakundwa,Namkunda,Nabera,Namangi,Nangasu,Naomba, Nambike, Nampingu, Namshitu, Namsi, Namwai, Namwasi, Nangena, Nanguji, Nanguma, Nankondo, Nanyika, Nanza, Nanzano, Nanzighe, Narindwa, Nasero, Nashumbwe, Natujwa, Navoneiwa, Navuri, Navushiku, Ngalakere, Nghuhia, Niendiwe, Nietiwe, Ntevona, Sangiwa,Shode, Yunesi.
Majina ya kiume:Bumija, Chali, Chaligha, Charo, Charema, Chedieli,Chuma, Elieseri, Eliesikia,Elinighenja,Elibariki,Elifazi, Elitumaini, Fue, Ghuheni, Gurisha, Ibwe, Igaria, Irema, Irigo, Irira, Kadio, Kadiva, Kajiru, Kakore, Kalage, Kalimbo, Kalinga (Jina hili pia lipo Mkoa wa Iringa),Kalutu, Kambaita (Jina hili lipo pia kwa Wachagga), Kaniki, Kanyempwe, Karia (Jina hili lipo pia kwa Wachagga), Kateri, Kazeni, Kazoka, Kejo, Kiandiko, Kiangi, Kiariro, Kideghedo (Same), Kideghesho (Mwanga), Kihara, Kijo, Kilave, Kileghe, Kileng'a, Kinenekejo (Wengine hufupisha na kuita Kejo), Kintungwa, Kipesha, Kisamo, Kisenge, Kitojo ,Koshuma, Kutua, Letei, Liana, Linga, Lukiko, Lukio,Lukungu, Lusingu, Macha (Jina hili lipo pia kwa Wachagga ambapo kwao ni Ukoo), Machwa, Madoffe, Maghembe (jina hili lipo pia kwa Wasukuma likiwa na maana ya majembe), Maliondo, Mapunjo, Mashuve, Mbajo, Mbasha, Mbazi, Mbonea, Mbuji, Mcharo, Mding'i, Mgheni, Mhando (Jina hili pia lipo mkoa wa Tanga), Minja (Jina hili pia lipo kwa Wachaga ambapo kwao ni Ukoo), Mkodo, Mkwavi, Mlavwasi, Mmari (Jina hili lipo pia kwa wachaga lakini maana zikiwa tofauti. Kwa Wapare lina maanisha mtafuta mali), Mnaro, Mndima, Mntambo, Mntindi, Mnyindo, Mrekwa, Mrimi, Mrinde, Mrindwa, Mrindoko, Mrio, Mroki, Mshigheni, Mtango, Mtengeti, Mtera, Mteti, Mwanyika (Jina hili pia lipo Mkoa wa Iringa), Mweri, Mweta, Mzangaze, Nachai, Ndago, Ngasu, Ngomoi (Same), Ngomuo (Ugweno), Nguve, Ngwijo, Niarira, Nisaghurwe, Nkima, Ntarishwa, Ntekaniwa, Nyange (Jina hili lipo zaidi kwa Wachagga lakini linatumika hata kwa wapare. Kwa Wachagga ni ukoo ambapo kwa Wapare ni jina tu la kawaida), Nzao, Nziajose, Nziamwe, Ojuku, Ombeni, Pekea, Ringo (Jina hili lipo pia kwa Wachagga ambapo kwao ni Ukoo), Sechome, Sechuma, Sefue, Semboja, Sempeho, Sempombe, Semu, Sengasu, Sengondo (Mwanga), Senguji, Senkondo (Same), Senkoro, Senzia, Senzota, Sevuri, Shaghude, Taseni, Tenga (Jina hili pia lipo kwa Wachagga ambapo kwao ni Ukoo), Tenshigha, Teri,Twazihirwa,Warema,Zihirwa , Zihirwani.
Ikumbukwe kwamba majina haya si ya koo bali ni majina ambayo Mpare yeyote anaweza akachukua au akamwita mtoto wake. Pia majina haya ni baadhi tu kati ya majina mengi ya Wapare yakiwa na maana tofauti tofauti.Tamaduni,mila na desturi za wapare zimekuwa zikifanana sana kwa koo karibu zote.Hapo kale wapare pia waliweza kutengeneza au kuifunga mvua kwa shughuli za jadi jambo ambalo wapo baadhi ya wapare ambao mpaka leo wanaweza.Kwa mfano Mtemi wa Same Mohammedi Kibacha Singo ambaye aliacha uongozi mara baada ya Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupiga maarufuku utawala wa jadi.Kiongozi huyu aliyefariki dunia mwaka 1981 alikuwa na ujuzi mkubwa wa kuleta mvua.Pia walikuwepo hata watu maarufu maeneo ya wilaya ya same ambao waliamini dawa fulani ambazo waliziweka shambani na hapo hakuna hata mdudu wala ndege atakayeweza kutua eneo hilo.Mambo haya na mengine mengi kwa sasa yanapotea kama siyo kuisha kabisa.Ngoma za jadi zilipigwa kwa matukio maalum kama kwenye jando au unyago,pia nyimbo za kipare zilitumika katika ngasu kama harusi na sherehe nyingine na kupendezesha tukio husika.Baadhi ya nyimbo huimbwa hadi leo hata kwenye sherehe za ukumbini na baadhi zimerekodiwa.Wapare walikuwa na utamaduni wa shughuli za sanaa kama methali,hadithi,maigizo n.k wakati wa m story itamaliziwa wiki ijayo usikose

No comments:

Umesoma hizi hapa