'peleka huko kazi yako si kujiuza tu'
'wewe hujatualia ni mapepe tuu'
'we unazani nisinge kuoa ungeolewa wewe?'
hayo ni baadhi ya maneno ambayo nimewasikia baadhi wa wanawake wenzangu wakilalamikia wanaume zao kuwatukana hivyo,kwa kweli akina baba haipendezi kumwambia mwanamke aliyekuzalia watoto malaya hata kama amekukosea!maneno mengine huwa hayafutiki moyoni haraka na yanapunguza mapenzi kwa kiasi kikubwa sana. Tujaribu kugombana kwa kutukia akili ni sio mioyo, tujaribu kutumia kauli ambazo zitajenga uhusiano na sio kubomoa ni hayo tu.

Angalizo; wapo pia wanawake wenye midomo michafu sana kwa wanaume au wapenzi wao hili pia laweza kuwa ni tatizo kwa jinsia zote.