Promote your business for free grow your business for life you don't need to spend more money anywhere.

THIS BLOG IS SPONSORED BY AHADIWAY ,ADVANTAGES FOR JOINING AHADIWAY BOON CAREER (ABC) CHAPTER = Employment opportunities within and outside the country. , Job experience , Self -employment , Field stations, part time jobs and chances to be trained.

Thursday, May 30, 2013

MUHIMBILI YATANGAZA MAMIA YA NAFASI ZA MADAKTARIHospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imetangaza mamia ya nafasi za ajira kwa idara tofauti, wakiwamo  madaktari bingwa na wauguzi wa vitengo, vikiwamo vya watoto na upasuaji wa moyo.

Takribani watu 488 wanahitajika kujaza nafasi hizo zilizotangazwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo katika maeneo mbalimbali hususan ya kitaalamu.
Miongoni mwa wanaohitajika ni madaktari bingwa daraja la pili  57 wa vitengo vya moyo, upasuaji, watoto, dawa za usingizi na mishipa.
Kati ya nafasi hizo zaidi ya 400, wanahitajika pia madaktari wa kawaida 85 ambao ni wa daraja la pili. 

Kwa mujibu wa tangazo hilo la  Mkurugenzi Mtendaji , madaktari  bingwa  wanatakiwa wawe  wamesajiliwa katika Baraza la Madaktari la Tanganyika.
Wanahitajika pia maofisa wauguzi 22 ambao kati yao, nafasi moja ni kwa ajili ya Ofisa Mwandamizi, 11 ni maofisa wa daraja la kwanza na 10 ni wa daraja la pili. 

Kwa upande wa maofisa wasaidizi, wanahitajika 10 wa daraja la kwanza na wengine 184 wa daraja la pili. Aidha, wanahitajika wataalamu saba kwa ajili ya kitengo cha mionzi.
Wataalamu wengine wanaohitajika ni wafamasia,  wauguzi,  maofisa afya na wataalamu wa maabara. 

Kulingana na tangazo hilo, nafasi hizo zinatakiwa haraka kutokana na waombaji kuelekezwa kutuma maombi kabla ya Juni 21.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, waombaji wanaofanya kazi katika taasisi za Serikali,  maombi yao yanapaswa kupitia  kwa waajiri na ajira zao zitahamishwa baada ya kuthibitishwa na Katibu Mkuu.

Ingawa wasemaji wa hospitali hiyo hawakupatikana jana kuelezea hali halisi ya rasilimaliwatu MNH, habari zilizowahi kuripotiwa na baadhi ya magazeti zilisema inakabiliwa na upungufu wa madaktari  bingwa wa upasuaji, hususan katika kitengo cha watoto.
Hata hivyo, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilipata kusema  upungufu huo wa madaktari bingwa, hauathiri shughuli za tiba katika kitengo hicho cha magonjwa ya watoto.

No comments:

Umesoma hizi hapa