Promote your business for free grow your business for life you don't need to spend more money anywhere.

THIS BLOG IS SPONSORED BY AHADIWAY ,ADVANTAGES FOR JOINING AHADIWAY BOON CAREER (ABC) CHAPTER = Employment opportunities within and outside the country. , Job experience , Self -employment , Field stations, part time jobs and chances to be trained.

Sunday, October 31, 2010

Ubalozi wa Tanzania

SHUKRANI

Marehemu Mchungaji Matiku Thomas Nyitambe


Familia ya Marehemu Mchungaji Matiku Thomas Nyitambe iishio Uingereza na Tanzania, kwa moyo mkunjufu, tunapenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, Jumuiya ya watanzania Reading na Slough ,Kanisa La wasabato (Angaza SDA Church -Reading), Madhehebu yote ya kidini hapa UK ,vyama vyote vya kisiasa,Waganga wote kutoka Mkoa wa Mara ,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na pia bila kusahau blog zote zilizo shiriki kutoa taarifa(Hakingowi,Issa Michuzi,Majid Mjengwa ,TZUK,Watanzaniaoslo,Musoma -tanzania ,wavuti n.k) , kwa kufanikisha shughuli zote za msiba wa Marehemu baba yetu Mchungaji Matiku Thomas Nyitambe ambaye alifariki Kutokana na ajali ya gari tarehe 3/October /2010 na hatimaye kuzikwa tarehe 9 /October/2010 kijijini kwake Kirongwe Tarime MkoaniMara.


Tunapenda pia kutoa shukrani nyingi kwa majirani,ndugu,jamaa na marafiki kwa misaada yenu ya hali na mali ambayo imewezesha familia ya marehemu walioko Uingereza kuweza kuwahi mazishi.


Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru kila mtu kipekee, tunasema tu kwamba Asanteni sana kwa michango yenu ya hali na mali ambayo ilisaidia katika mipango na mikakati yote ya kuuhifadhi mwili wa Marehemu hadi kuzika.


Hatuna cha kuwalipa bali tunamwomba Mwenyezi Mungu awajalie na kuwazidishia mibaraka katika shughuli zenu za kila siku.Tumeambatanisha picha za ajali .


Sisi tulimpenda sana Marehemu Nyitambe lakini


Mwenyezi Mungu amempenda zaidi,


Jina la Bwana lihimidiwe.


Asanteni sana


Amen

No comments:

Umesoma hizi hapa