Promote your business for free grow your business for life you don't need to spend more money anywhere.

THIS BLOG IS SPONSORED BY AHADIWAY ,ADVANTAGES FOR JOINING AHADIWAY BOON CAREER (ABC) CHAPTER = Employment opportunities within and outside the country. , Job experience , Self -employment , Field stations, part time jobs and chances to be trained.

Thursday, May 24, 2012

kufanya mapenzi kinyume na maumbile

watu wengi wanajikuta ni waathirika wa mchezo wa kudandia ukuta kwa sababu kadhaa. Mosi ni stori za vijiweni, kwamba wanaume wanadanganyika mno na habari za kusikia kwa wengine.
Wapo wanaoingia huko kwa sababu ya kulazimishwa na wapenzi au waume zao. Kuna wanawake wanaoamua kujitoa mhanga kwa ajili ya kutibu shida za maisha. Pia lipo kundi linaloamini kwamba kwa kuwaruhusu wanaume wao kuwadandia ukuta, watawafanya wawapende zaidi.


Yapo maneno ya kuwa tendo likitekelezwa taratibu, pia matumizi ya mafuta yanaweza kuleta usalama. Mtandao wa womenanswers.org


unalizungumzia hilo lakini unachambua kwa upana kwamba mlango husika unaunga kwenye uti wa mgongo, hivyo ni lazima ulindwe kwa sababu ukiharibiwa husababisha ulemavu wa maisha.

Unaeleza kuwa mlango huo haupo kwa ajili ya kupitisha kitu kutoka nje, hivyo ukitumiwa ndivyo sivyo ni rahisi kuchanika, kumsababishia maumivu makali mhusika pamoja na kuvuja damu.

Yapo pia maneno kwamba ni rahisi mwanaume kufika mwisho anapopita mlango huo kwa sababu ni mdogo na unabana. Hayo yanaibua upofu wa kuona ukweli kuwa mwisho wa tendo ni sawa na kumsababishia ulemavu mtendwa.


“Mimi ni mke wa mtu, naomba unihifadhi jina. Mume wangu alidhani sifa kuniingilia kinyume na maumbile lakini nilipata usumbufu mkubwa wakati wa kuzaa. Niliambulia matusi kutoka kwa manesi kwani nilishindwa kumsukuma mtoto, hii yote ni kwa sababu ya mchezo huo”.

Nikifafanua SMS ya Mama X ni kuwa athari nyingine ya mapenzi ya kudandia ukuta ni wakati wa kuzaa. Kitaalamu mwanamke anayefungua mlango wa nyuma, inapofika wakati kumsukuma mtoto nao hufunguka na kukaa wazi, hivyo kumsababishia usumbufu mzazi na kuchoka haraka.

Kwa hali hiyo, mtoto hushindwa kutoka kwa urahisi kwenye njia yake kwa sababu mzazi hushindwa kumsukuma inavyotakiwa. Hilo linapotokea, wakunga huwa wakali dhidi ya wazazi na matokeo yake kwa wale wasio na staha ni kuwatolea lugha chafu.


Kuna simulizi kutoka Zanzibar kuwa mabinti wadogo huingia katika mchezo wa kuruhusu wageni kwa mlango wa nyuma ili kulinda bikira zao, kwamba heshima yao kwenye ndoa ni kukutwa ukiwa mwali. Wajuzi wa mambo wanasema ‘katabia’ hako Zenji kamekolea kweli kweli.

Yapo mafundisho ya kidini, ipo mifano ya Sodoma na Gomora ndani ya vitabu vya dini. Hii ina maana kuwa yeyote ambaye anajihusisha na mchezo huo, hafanyi kile kinachompendeza Mungu wake.

ATHARI YA KUDANDIA UKUTA KIAFYA
Pointi kuu ni kwamba watu wanaokimbilia mlango huo wako kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa kwa sababu kitaalamu, njia hiyo ni rahisi kupitisha Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Inaeleweka kwamba, mwanamke hawezi kupata ujauzito kwenye njia hiyo, lakini nyongeza ya kitaalamu ni kuwa mlango wa nyuma kwa kawaida huwa una wadudu wenye maradhi (bacteria) ambao humshambulia mwanaume anayepita huko.

Hii ina maana kuwa tendo hilo hata kama litafanywa kwa kondomu, bado athari yake ni kubwa, bakteria ni wengi eneo hilo kwa ajili ya kulinda mlango husika. Hii ina maana kuwa hata kama nyote wawili mmepimwa na mmegundulika mpo salama lakini wadudu wa maradhi siku zote wapo kwenye njia hiyo.

Mapenzi ya kudandia ukuta, pia hutoa athari kwa mwanaume katika mfumo wa mkojo. Hii ni kwamba kuna urahisi wa kuingiliwa na chembechembe hatari na tatizo likiwa kubwa kumsabishia mhusika kwenda haja ndogo kwa kutumia mipira.

Ushauri ni kwamba mlango huo haupo kwa ajili ya mapenzi, hivyo kwa mwanamke ni mateso kuliko raha, pia kuchanika kwa urahisi kwa sababu njia hiyo haitanuki kama ilivyo kwa barabara ya kawaida (mlango wa kawaida).

Utafiti uliofanywa na mtandao wa womenask.com unaweka wazi ripoti yake kwamba mtu aliyezoea mchezo wa kupitisha mgeni kwa mlango wa nyuma, baadaye huathirika mno na hulazimika kuvaa nepi. Hii ni kwa sababu misuli yake hulegea, hivyo kushindwa kudhibiti haja.

Mtandao huo unashauri pia kwamba ikiwa mwanaume atapita mlango wa nyuma, hatakiwi kurudi mbele kwa sababu kwa kufanya hivyo,

anaweza kumuambukiza mwenzake wadudu wa maradhi ambao wameelezwa hapo juu kwamba wanapatikana kwenye mlango wa nyuma.

No comments:

Umesoma hizi hapa