Promote your business for free grow your business for life you don't need to spend more money anywhere.

THIS BLOG IS SPONSORED BY AHADIWAY ,ADVANTAGES FOR JOINING AHADIWAY BOON CAREER (ABC) CHAPTER = Employment opportunities within and outside the country. , Job experience , Self -employment , Field stations, part time jobs and chances to be trained.

Friday, December 21, 2012

Lulu Michael aingia mtaani

Lulu.Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam LEOimemuachia msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael Kimemeta, maafuru kama Lulu, kwa dhamana baada ya kupitia vifungu vya sheria. Mtandao wawww.habarimasai.com unaripoti kwamba uamuzi huo umetolewa asubuhi ya LEO na mahakama hiyo.
Awali Mkurugenzi wa Mashtaka  nchini (DPP), alibadilisha mashtaka na Lulu kutuhumiwa kuua bila kukusudia.
Kutokana na mabadiliko hayo sasa Lulu ameepuka adhabu ya kunyongwa  hadi kufa kwa tuhuma za kumuua aliyekuwa msanii maarufu nchini, Steven Kanumba.
Sasa Lulu endapo atapatikana na hatia, adhabu yake itakuwa ni kifungo cha maisha au kuachiwa huru.
Hali hiyo inatokana na kifungu cha 196 cha kanuni za adhabu ya kosa la kuua  bila kukusudia na anayepatikana na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha, miaka kadhaa au kuachiwa huru.

No comments:

Umesoma hizi hapa