Promote your business for free grow your business for life you don't need to spend more money anywhere.

THIS BLOG IS SPONSORED BY AHADIWAY ,ADVANTAGES FOR JOINING AHADIWAY BOON CAREER (ABC) CHAPTER = Employment opportunities within and outside the country. , Job experience , Self -employment , Field stations, part time jobs and chances to be trained.

Friday, May 25, 2012

Ni zaidi ya Ngono!

Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo huwa wengi hatuvitilii maanani kwa maana kuwa tunavidharau kwavile tunadhani kuwa havina umuhimu wowote ktk uhusiano wetu wa kimapenzi iwe ktk ndoa au “ushirika” kuishi pamoja bila makaratasi ya kisheria/kidini kwa tafasiri yangu binafsi usije ukainadi mtaani, sawa!

Sehemu kuwa ya jamii inafikiri kuwa ukiwa msafi wa mwili ofcoz, mazingira (mahali unapoishi/ulipo), mpanga bajeti mzuri, mpishi wa uhakika na mshiriki mzuri wa tendo la ndoa/ngono basi uhusiano wako unakwenda ktk njia iliyonyooka nikiwa na maana hakuna kona wala mabonde na “mupenzi” kamwe hatolalamika.

Heheheh in ur dreams! Asipokulalamika basi atalalamikia huko kwingine akirudi nyumbani anajifanya kama vile hakuna jambo linalomsumbua/udhi which is good kama wewe sio msikilizaji mzuri, mana’ke atakuwa amejisaidia kuepusha mzozo ambao unaweza kusababisha mihangaiko ya akili na mwili (stress).


Kuna vitu vidogo kama vile muonekano wako ukiwa nje ya nguo, mana’ke sote twajua nguo zaficha vingi atii…..sasa je umependeza na jeans yako ukiiondoa utabaki umependeza au ndio vile? Hilo mosi.


Pili ni swala dogo kama kubadili shuka kitandani na uchaguzi wa rangi hizo au hata kubadili mpangilio wa kitanda kutoka ukutani kuwa katikati, kuongeza mito midogo n.k.


Aina ya manukato unayotumia, kale ka mchezo ka kubadili na kujaribu kila manukato yanayoingia mjini ni ushamba…….(unless ofcoz umeachana na jamaa na hutaki kumbukumbu yake kwa vile alikuwa akivutiwa na manukato Fulani), sasa basi jaribu kuwa na aina mbili tofauti hasa kama wewe na mpenzi wako ni watu wa “outings” moja iwe ya kila siku na nyingine iwe ya jioni siku unayoamua kuwa-sexy au unapotoka.


Nitakupa mfano well, ndio nazipenda na nizitumia mimi…..Eden (harufu yake imechangamka) ni ya kila siku/kazini na Organza (harufu yake imetulia) ni ya jioni/kutokea/tayari kwa mambo Fulani…..sikutumi ukanunue hizi ila nimekupa tu mfano unaweza ukanunua zile unazozipenda. Hili basi ni la tatu.


Na nne, ni kubadili aina za mitindo ya chupi unazovaa, haijalishi una umri gani au unaumbile kubwa kiasi gani siku moja-moja unampigia kale kadogo alafu kama vipi wewe unapenekua tu kidogo kitu na box…..kuanzia siku hiyo anaweza akawa anakutaka ukivaa kachupi kadogo badala ya bukta ulizo zoea, na wewe uliezoea “tudogo” jaribu kumpigia boxer yake….hahahaha, siku moja moja piga zile zinazofunik matako yote au zile za ki-boyish.


Usifunike kichwa chako kila unapokwenda kulala, natambua kuwa kunamtindo mingine ya nywele inakubidi ufunge tambala ili isivurugike na pia najua kuwa vitambaa vya satini vinasaidia kutuza unyevy-nyevu wa asilia wa nywele nakuzifanya ziwe na afya lakini, sio mbaya kama ukiziachia nywele hizo wazi siku moja moja ili mume/mpenzi akiamka aone ulivyo mzuri bila lemba ambalo amelizoea kila siku. Hilo ni la tano.

No comments:

Umesoma hizi hapa