Promote your business for free grow your business for life you don't need to spend more money anywhere.

THIS BLOG IS SPONSORED BY AHADIWAY ,ADVANTAGES FOR JOINING AHADIWAY BOON CAREER (ABC) CHAPTER = Employment opportunities within and outside the country. , Job experience , Self -employment , Field stations, part time jobs and chances to be trained.

Monday, April 30, 2012

NANI ANGEJINASUA HAPA? TOWN BALAA JAMANI (KAA CHONJO)

Unatoka kazini ukiwa umechoka na kazi ngumu za ofisi zisizoisha. Umeamua kwenda karibu na kituo cha daladala ili ujirudie zako nyumbani. Nyumbani ni mbali, muda unazidi kwenda na hakuna dalili ya daladala kuja mapema.
Unaamua kutembea kidogo ili daladala ikukutie njiani. Ukiwa unatembea kwa uchovu unaotokana na uzito wa begi la laptop uliyoibeba na mawazo chungu mzima kuhusu familia na kazi, mara mbele yako kidogo inasimama gari ndogo mpya kabisa ikiwa tinted!

Kioo kinashuka na unamwona msichana mrembo anachungulia na kukusemesha “Mambo kaka”, ukiwa bado kwenye mshtuko mkubwa wa kusalimiwa na msichana huyo mwenye tabasamu la haja, unaitikia kwa kujiumauma, “aah poa tu dada”. “Unaelekea wapi kwani?”Anakuuliza tena kwa sauti ile ile yenye mvuto na inayosindikizwa na tabasamu toka kwa msichana anayeonekana kutojua maana ya neon ‘shida’.

Ukiwa umeanza kujiamini kidogo unamwambia unakoelekea. Anakuambia yeye anaenda mbele ya huko uendako na angependa akusogeze. Kimoyo moyo unajiongelesha “hili zali” na kutojiuliza mara mbilimbili.
Unazunguka upande wa pili wa gari na unaingia ndani. Unapoingia ndani unakutana na halufu nzuri ya perfume ya Beyonce Pulse! Halufu yake na mchanganyiko wa AC ya ndani ya gari lake inakupeleka paradise inayojengwa kwa muda mfupi ndani ya mawazo yako mwenyewe.

Anakuangalia kwa upole na kuisafisha siti unayotakiwa kukaa na kukukumbusha kufunga mkanda. “Unaonekana umechoka sana kaka, pole na kazi” Anakusemesha huku macho yake yakiwa mbele kutokana na kuiondoa gari la kuanza safari. Ukiwa bado unautafakari urembo wake kama wa malaika unamjibu “Asante”. Anakuambia huna haja ya kukaa na begi lako miguuni na unaamua kuliweka kwenye siti za nyuma ya gari.

“Unaitwa nani” anakuuliza kwa tabasamu lingine linalokufanya ugundue kumbe anabonyea shavuni pia. Unashangaa ukijikuta unaingiwa na woga tena, unamjibu kwa kumwambia majina yako yote mawili lakini macho yako yakiwa yametazama katikati ya kiti chake na chako ambako kumewekwa simu mbili za gharama kabisa, iphone 4s nyeupe na Samsung GALAXY S II nyeusi.

“Mimi naitwa Lynette”, anajitambulisha kwako. Unamwambia jina lake zuri na mnacheka kwa pamoja. Baada ya dakika kama kumi na tano ya safari yenu mnajikuta mmezoeana sana. Anakupa story zake na wewe unampa zako na vicheko vinatawala ndani ya gari.

Mnafika sehemu kuna maduka kadhaa na anakuambia kiu kimemkaba sana na ameshindwa kuvumilia. “Samahani George naomba unichukulie maji makubwa ya Kilimanjaro hapo mbele”. Anakupa shilingi 2,000 na unaonesha kufurahia kutumwa maji na msichana mrembo kama yeye.

Unaenda dukani. Unapofika unanunua maji kama anavyotaka lakini unajishauri ununue kitu kingine kidogo tu kama surprise kwake na kuonesha shukrani kwa wema na uchangamfu wake kwako. Unaamua kununua chocolate za shilingi 5,000. Unarudi pale mlipoegesha gari lakini unashangaa hulioni! Baada ya dakika kama kumi unagundua kuwa ameshaondoka na tayari umetapeliwa!!!!

No comments:

Umesoma hizi hapa