Promote your business for free grow your business for life you don't need to spend more money anywhere.

THIS BLOG IS SPONSORED BY AHADIWAY ,ADVANTAGES FOR JOINING AHADIWAY BOON CAREER (ABC) CHAPTER = Employment opportunities within and outside the country. , Job experience , Self -employment , Field stations, part time jobs and chances to be trained.

Sunday, October 17, 2010

Parachichi: Kinga ya ugonjwa wa moyo na saratani ya matiti

Parachichi: Kinga ya ugonjwa wa moyo na saratani ya matiti


Kama yalivyo matunda yote kwa ujumla kuwa yana faida sana katika mwili wa binadamu, vivyo hivyo na Parachichi. Tunda hili lina uwezo mkubwa wa kupambana na maradhi hatari ya moyo na sataratani ya matiti kutokana na virutubisho ilivyonavyo.

Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi juu ya tunda hili, lina kirutubisho aina ya Aloic Acid ambayo ni aina fulani ya mafuta mazuri yanayosaidia kushusha kolestrol mwilini. Katika utafiti mmoja waliofanyiwa watu kadhaa waliokuwa na matatizo ya kolestro mwilini, baada ya kutumia maparachichi kwa muda wa siku saba, walionesha mabadiliko mazuri katika afya zao kwa kupungua kiwango cha kolestro mbaya mwilini.

Aidha, parachichi lina kiwango kikubwa sana cha madini aina ya potasium ambayo ni muhimu sana katika kuimarisha mzunguruko wa damu mwilini. Inaelezwa kwamba ulaji wa kiwango kikubwa cha madini ya potasium, hutoa kinga madhubuti dhidi ya magonjwa yatokanayo na mzunguruko mbaya wa damu mwilini, kama vile ugonjwa wa moyo, shinikizo la damu na kiharusi.

Mbali ya madini hayo, parachichi lina virutubisho vingine kama vile Folate (Folic acid) ambacho ni muhimu sana kwa afya na ustawi wa moyo, kwa maana hiyo watu ambao wanakula sana vyakula kama parachihi vyenye kirutubisho hicho, watukuwa salama dhidi ya magonjwa ya moyo au kiharusi kwa asilini 55.

Kirutubisho kingine kinachopatikana kwa wingi kwenye parachichi ni Fatty Acids, ikiwemo Oleic Acid. Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, imedhihirika kwamba virutubisho hivyo ni kinga tosha dhidi ya saratani ya matiti. Kwa maana nyingine, wanawake wanaokula kwa wingi maparachichi, wanaipa miiili yango kinga dhidi ya saratatani hiyo ambayo hivi sasa imekuwa tishio miongoni mwa wamawake wengi nchini.

Parachichi linaweza kuliwa kama mtu atakavyopenda, wapo watu wanaopenda kula bila kuchanganya na kitu kingine, lakini pia parachichi linaweza kuliwa kwa kupaka kwenye mkate badala ya Blue Band. Halikadhalika parachichi linaweza kuliwa kwa kuchanganya na nyanya, vitunguu, ndimu na chumvi kidogo kama kachumbari ya kipekee au kunywa juisi yake.

VIRUTUBISHO VYA PARACHICHI
Kwa ujumla, parachichi ni chanzo kizuri cha Vitamini K, Vitamini B6 na Vitamini C. Aidha tunda hili lina kiwango kizuri cha virutubisho aina ya Folate, kopa na kambalishe (Fiber).

Fiber ni muhumu katika kuwezesha mtu kupata choo laini na bila matatizo. Bila kusahau kwamba tunda hili ni chanzo kizuri pia cha madini ya Potasiamu: ina kiwango kikubwa kuliko hata ndizi.

Ingawa parachichi ni tunda, lakini lina kiwango kikubwa cha mafuta (fats) ambayo yanakadiriwa kuwa kati ya asilimia 71 – 88, kiwango ambacho ni cha juu kwa asilimia 20 ukilinganisha na matunda mengine. Kwa wastani, parachichi moja lina gramu 30 za mafuta, lakini kati ya hizo, gramu 20 ni za mafuta mazuri kiafya (Monounsaturated fats na Aloic Acid) ambayo husaidia kujenga afya bora mwilini.

Utafiti zaidi kuhusu tunda hili unamalizia kwa kusema kwamba parachichi lina takribani aina 20 za Vitamin, madini na virutubisho muhimu (Phytonutriens) ambavyo hutuo kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mengi hatari. Baadhi ya Vitamini zilizomo na asilimia zake kwenye mabano ni pamoja na Vitamin E (4%), Vitamin C (4%), Folate (6%), Fiber (4%), Iron (2%) na Potasium (4%).
Kwa ujumla tunda la Parachichi lina faida nyingi kiafya na tunatakiwa tuyale kwa wingi, kwa faida ya miili yetu
!

No comments:

Umesoma hizi hapa