Promote your business for free grow your business for life you don't need to spend more money anywhere.

THIS BLOG IS SPONSORED BY AHADIWAY ,ADVANTAGES FOR JOINING AHADIWAY BOON CAREER (ABC) CHAPTER = Employment opportunities within and outside the country. , Job experience , Self -employment , Field stations, part time jobs and chances to be trained.

Sunday, October 17, 2010

Mihogo michungu

Konzo ni Sumu inayopatikana katika Mihogo michungu mibichi.
Hayo yamewekwa bayana na Ofisa Lishe wa Idara ya Chakula ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Sakina Lweno ametoa tahadhari hiyo Dodoma mwishoni mwa wiki aliseyasema hayo katika mafunzo ya kilimo kwa wakulima akisisitiza kuwa Sumu hiyo inasababisha mlaji kupooza mwili
Lweno aliendelea kusema muathirika wa sumu hiyo hupooza kuanzia kiunoni kushuka chini na kwamba sumu hiyo hufanya kazi polepole na madhara kutokea baada ya kutumia mihogo mibichi kwa muda mrefu . Ugonjwa huo haufahamiki na watu wengi na uligundulika kati ya mwaka 2003 na 2004 wakati wataalamu wa wizara hiyo walipotembelea Mkoa wa Mtwara.
Kutokana na ongezeko la biashara ya mihogo mibichi katika jiji la Dar es Salaam wakazi wake nao wapo katika hatari ya kupata tatizo hilo kwa sababu mihogo hiyo huwa ya kutafunwa mibichi
Tahadhari imetolewa kwa jamii kuepuka kula aina hiyo ya mihogo kwa sababu bado utafiti unaendelea kufanyika kwamba ni kwa kiasi gani sumu hiyo inamuathiri mlaji huyo.

No comments:

Umesoma hizi hapa