we're trying to accomplish something.only gossip work for us.contact us on nitonyeni@gmail.com
Tuesday, February 1, 2011
bongo kazi kweli kweli
KAZI KWELI: "DOWANS,KUKU ANAYEKIMBIA NA PANZI WAKE MDOMONI"
HUTOKEA, kuku akimdaka panzi mdomoni, basi, ukimwandama ukimpigia kelele. Kuku huyo atakimbia na panzi wake mdomoni . Mara ile atakapoona umesitisha kumfukuza , na kelele pia. Basi, kuku huyo, taratibu ataanza kumla panzi wake.
Lakini, kama utaendelea kumwandama na kumpigia kelele, hutokea, kwa kuku anayekimbia na panzi mdomoni, kumtema panzi ili kuandamwa huko kwishe.
Dowans ni kama kuku na panzi wake mdomoni. Alishamdaka, kabla hajaanza kumla, Watanzania tumeamka na kuanza kumwandama Dowans huku tukimpigia kelele.
Kuku Dowans ameonyesha dalili za kuweweseka. Tukiongeza kupiga kelele, basi, upo uwezekano wa Dowans kumtema panzi.
Naam. Tuendelee tu kupiga kelele za ’ HATULIPI!, HATULIPI! ’- NON SI PAGA! Kwa Kiitalia. Yumkini panzi aliyemdomoni mwa Dowans anaweza kutemwa! Itakuwa nafuu kwetu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Umesoma hizi hapa
-
KUJISTIRI ndio hasa lengo la awali la uvaaji. Na kupendeza ni jambo la pili ambalo limekuwa likizingatiwa sana na wanawake. Lakini ili haya...
-
Wapare ni kabila kutoka milima ya Pare, Mkoa wa Kilimanjaro, kaskazini mwa nchi ya Tanzania. Lugha yao ni Kipare (au Chasu). Wapare wanat...
-
watu wengi wanajikuta ni waathirika wa mchezo wa kudandia ukuta kwa sababu kadhaa. Mosi ni stori za vijiweni, kwamba wanaume wanadanganyika ...
-
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali mjini Dodoma wameoza kwa matukio machafu ya ngono.. Uchunguzi wetu umebaini kuwa siyo kil...
No comments:
Post a Comment