Promote your business for free grow your business for life you don't need to spend more money anywhere.

THIS BLOG IS SPONSORED BY AHADIWAY ,ADVANTAGES FOR JOINING AHADIWAY BOON CAREER (ABC) CHAPTER = Employment opportunities within and outside the country. , Job experience , Self -employment , Field stations, part time jobs and chances to be trained.

Saturday, October 9, 2010

MAPENZI!!!! TUNAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE?

Salute to women Kuna tukio nililiona MAISHANI:KKUTOKA KWA WISE MAN James ahadi
Acheni niwape heshima iliyotukuka wanawake woote; IMAGINE: ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza anakuelewa anakusamehe halafu anasahau!!!
UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka na kulia sana. Anakuchukia lakini baadaye anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo. Kama ni kuchukiwa atachukiwa mtoto, si wewe uliyefanya umalaya! UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI: Anakukaribisha, anakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila manung'uniko.
UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER: Anakuandalia staftahi (saa nyingine unagoma kutumia staftahi yake unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala halalamiki!
CHAKULA CHA USIKU: Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hamna maandalizi unamuumiza. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena inaweza tokea hii; hana kinyongo!
UNAJIANDAA KWENDA KIBARUANI: Unakuta kashakuandalia viwalo, suruwale imenyooshwa kama ya askari trafiki, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi! Ulichomuudhi jana kashasahau na kukusamehe!
UNAMPA UJAUZITO: Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto anakuachia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena!
Na mengine meeeeengi sana wanafanyiwa hawa watu lakini WANASAMEHE, WANAVUMILIA! Ni watu muhimu sana hawa watu maishani mwangu!
HIVI INGEKEWA WANAUME  TUNAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE?
Kwa leo acheni tu niwape heshima zao wanawake wote:
I SALUTE AND LOVE THEM WOMEN!

1 comment:

Anonymous said...

James hapo umenena,wanawake sisi ni watu wa kusamehe i wish wanaume wangekua wanatuthaimi kama sisi tunavyowathamini na kutupenda,but how many they are thinking about that?how many na wao wanajua ni kiasi gani wanatuumiza lakini tunasamehe??Mungu waangamize wanaume wanaonyanyasa wanawake au wahukumu sawa sawa na mapenzi yako..

Umesoma hizi hapa