Promote your business for free grow your business for life you don't need to spend more money anywhere.

THIS BLOG IS SPONSORED BY AHADIWAY ,ADVANTAGES FOR JOINING AHADIWAY BOON CAREER (ABC) CHAPTER = Employment opportunities within and outside the country. , Job experience , Self -employment , Field stations, part time jobs and chances to be trained.

Thursday, October 14, 2010

Je?mwanamke anapaswa kutunzwa hata kama ana kipato

Jinsia ni suala linalohusu maendeleo kwa sababu kutokuwepo kwa uwiano na usawa kama ilivyo sasa katika jumuiya, kunaizuia jamii kutambua uwezo wake kamili katika shughuli zote zinazohusu maendeleo ya uchumi, jamii na maeneo ya siasa. 
Serikali iko mbioni kuhakikisha kuwa masuala ya jinsia yanaunganishwa  katika kutayarisha mipango na bajeti ili kuimarisha uhusiano baina ya wanaume na wanawake ambao ndiyo unatoa msukumo kwa maendeleo. Kwa hiyo, pasikuwepo uhusiano imara kwa pande hizo mbili kasi ya maendeleo itapungua. 
Dira ya Maendeleo ya 2025 ya Tanzania inalengo la kuwapatia watu wake hali ya juu ya maisha, kufanikiwa katika kupata utawala bora wa kuheshimu sheria pamoja na kuendeleza uchumi imara na wa ushindani.  Ili kufanikiwa kuleta usawa wa jinsia na kuwapa uwezo wanawake katika maeneo ya jamii, uchumi, uhusiano wa siasa na utamaduni lazima yatiliwe maanani.  Jinsia imewekewa kipaumbele katika masuala yote ya Maendeleo ili kukuza uchumi wa Taifa, masuala ya siasa na utamaduni lazima yaangaliwe.  Jinsia ni mkondo mkuu ambao vipengele vyote vya maendeleo hupita ili kuimarisha uchumi wa Taifa, siasa na masuala ya jamii na utamaduni.  
Nchini Tanzania inakadiriwa kwamba wanawake hasa wa vijijini wanatoa asilimia 80 ya wafanyakazi katika eneo la kijiji na hivyo kutoa asilimia 60 ya chakula kinachozalishwa.  Ingawa wanawake ndiyo wazalishaji wakubwa wa mazao ya biashara, mazingira hayawaruhusu kumiliki mali zao.  Wanawake hawana maamuzi juu ya masula ya uzazi, kwa mfano wanawake wengi hawana uwezo wa kuamua idadi ya watoto katika familia ingawa wao ndiyo wenye jukumu kubwa la kulea mtoto. 
Jinsia katika mfumo wa ajira kwa shughuli za kilimo au zisizo za kilimo nchini Tanzania imebadilika katika kipindi cha miaka kumi iliyopita kwani wanawake wengi zaidi wanajishughulisha na masuala ya biashara na wanawajibika zaidi katika kuchangia fedha kusaidia mahitaji ya nyumbani.  Wanawake wako mstari wa mbele katika kupanua biashara ndogo ndogo ambazo hujulikana kama sekta isiyo rasmi.

No comments:

Umesoma hizi hapa