Kigogo mmoja wa kampuni tangu ya uingizaji na uuzaji wa mafuta nchini (jina tunalihifadhi) Jumanne ya wiki iliyopita alijikuta akikumbwa na maswahibu mazito baada ya ‘kuparalaizi’ akiwa anafanya tendo la ndoa.
Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, ambaye hakupenda jinalake kuandikwa gazetini, tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa 11.00 katika nyumba ya kulala wageni ya Masco iliyopo Temeke jijini Dar es Salaam.
Habari zinadai kuwa, kigogo huyo alitinga katika gesti hiyo na kukodi chumba namba 9 akiwa na hawara yake aliyejulikana kwa jina moja la Kibibi.
Ilidaiwa kuwa mwanamke huyo anayeishi eneo la Temekealitinga na mpenzi wake kwa lengo la kupeana raha lakini katika hali ya kushangaza wakiwa katikati ya tendo, kigogo huyo alianza kulalamika ya kuwa anahisi upande wake wa wa kushoto unapoteza nguvu.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa baada ya kigogo huyo kulalamika hivyo, hawara yake alisitisha zoezi walilokuwa wakifanya kisha kuanza kuchunguza kilichokuwa kikimsibu mpenzi wake ndipo alipobaini jamaa alikuwa ‘ameparalaizi’ upande wote wa kushoto.
Kutokana na hali hiyo Kibibi alichukuwa simu ya kigogo huyo na kuanza kupekuwa majina yaliyokuwemo na kufanikiwa kuona jina lililoandikwa ‘wife’ ambapo alimpigia na kumfahamisha yaliyojiri na eneo walilokuwepo kisha alitoweka.
“Kibibi alitoka chumbani akiwa amechanganyikiwa, tulimuuliza kilichomkumba akadai kuwa kigogo aliyekuwanaye ‘ameparalaizi’ ghafla, hivyo amempigia mkewe kumfahamisha,” kilisema chanzo hicho.
Aidha, chanzo hicho kiliongeza kuwa kimada huyo alisema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kuona kigogo huyo anashindwa hata kuongea.
Habari zaidi zinasema kuwa mke wa kigogo huyo alikwendaKituo cha Polisi cha Chang’ ombe na kutoa taarifa ambapo askari walikwenda eneo la tukio na kumkuta akiwa hoi.
Chanzo hicho kilisema kuwa askari hao kwa kushirikiana na watumishi wa gesti hiyo, walimchukuwa kigogo huyo na kumpeleka katika Hospitali ya Hindu Mandal kwa matibabu.
Kwa mujibu wa habari hizo, kigogo huyo alilazwa na kupatiwa matibabu hadi Alhamis ya wiki iliyopita ambapo alihamishiwa katika Hopitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Temeke, Emmanuel Kandihabi akiongea na mwandishi wetu alisema kuwa taarifa hiyo haijapata lakini aliahidi kuifanyia kazi.
No comments:
Post a Comment