MAZISHI YAKIENDELEA
WAOMBOLEZAJI WAKIWA MBELE YA KABURI LA MAREHEMU HUYO
MRATIBU WA POLISI ARUSHA, HAMIS WARIOBA
Na Idd Uwesu/Mpwaji Arusha yetu
Hatimaye mazishi ya mtu mwenye ulemavu wa ngozi aliyeuwa kinyama wilayani Arumeru mkoani Arusha miezi miwili iliyopita yamefanyika katika makaburi ya Njiro jijini Arusha.
Mazishi ya mlemavu huyo ambaye hakuweza kutambuliwa kutokana na kuchunwa ngozi na kuondolewa baadhi ya viungo vyake yamefanyika chini ya usimamizi wa Chama cha Maalbino Tanzania TAS na Shirika la Under the same sun Tanzania
Mwanahabari wetu Idd UWESU anataarifa zaidi.
Akiongea wakati wa mazishi hayo Mkurugenzi wa shirika la Under the same sun Tanzania, Vicky Ntetema amesema kuwa jukumu la kuwalinda walemavu wa ngozi nchini ni jukumu la kila mmoja na sio kuliachia jeshi la polisi pekee au serikali. Amesema jamii ihakikishe walemavu hao wanalindwa na kuthaminiwa kama binadamu wengine.
Ameongeza kuwa mauaji hayo ya kinyama ni lazima yakomeshwe na kwamba wale wote waliohusika na unyama huo kuhakikisha wanakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria. Amesema jamii ya kitanzania haina budi kuhakikisha inashirikana na jeshi la polisi kuhakikisha watu hao wanakamatwa.
Insert 1……Mkurugenzi UTSS Tanzania, Vicky Ntetema
Nae mwenyekiti wa mkoa wa Chama cha Maalbino Tanzania, Godson Mollel amesema wanalaani vikali tukio hilo na kuitaka serikali na mashirika mengine kukisaidia Chama chao ili kiweze kutembea maeneo mengi zaidi kuendelea kuelimisha jamii hasa za vijijini kuhusu imani hizo potofu ambazo ndizo chanzo kikubwa cha mauaji hay
Insert 2……Mwenyekiti TAS Arusha, Godson Mollel.
Kwa upande wa Jeshi la polisi, Mrakibu wa Polisi mkoa wa Arusha Hamis Warioba amesema Jeshi hilo hivi sasa linaendelea na uchunguzi na kwa mba halitasimama mpaka lihakikishe watu waliohusika na mauaji hayo wanakatamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.
Insert 3……. Mrakibu wa Polisi mkoa wa Arusha, Hamis Warioba
Mwili wa mlemavu huyo uliokotwa tarehe 29 mwezi mei mwaka huu pembezoni mwa nyumba ya mkazi mmoja wilayani Arumeru. Mazishi hayo pia yalihudhuriwa na Mariamu Staford mlemavu wa ngozi ambaye alikatwa mikono yake alipovamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwao huko Ngara.CREDITS: ARUSHA
No comments:
Post a Comment