Promote your business for free grow your business for life you don't need to spend more money anywhere.

THIS BLOG IS SPONSORED BY AHADIWAY ,ADVANTAGES FOR JOINING AHADIWAY BOON CAREER (ABC) CHAPTER = Employment opportunities within and outside the country. , Job experience , Self -employment , Field stations, part time jobs and chances to be trained.

Saturday, June 30, 2012

“KUPIGWA KWA Dk. ULIMBOKA, KAMA NI SERIKALI BASI TUTAKUWA NI WATU WA AJABU SANA”, PINDA




WAZIRI MKUU Mizengo Pinda
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda , amesema tukio la kupigwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dk Stephen Ulimboka, lina utata na kuongeza kuwa uchunguzi utakaofanywa na vyombo vya usalama ndio utakao maliza utata huo.
Pinda aliyasema hayo Ijumaa Juni 29, 2012 bungeni alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe (CHADEMA), ambaye alitaka kujua hatua ya serikali ya kutotoa tamko wakati juzi alitoa kauli nzito ya ‘liwalo na liwe’ kuhusu mgomo wa madaktari na kuibua hofu kubwa kwa wananchi, serikali inalieleza nini taifa kuhusu hali hiyo na inafanya nini kumaliza mgomo huo katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo.
Akijibu swali hilo, Pinda kwanza alikiri kuahidi kutoa tamko la serikali akitumia neno la “liwalo na liwe’, lakini akadai kuwa serikali haitaweza kutoa tamko hilo tena baada ya kupata ushauri wa kisheria kwa kuwa jambo hilo liko mahakamani.
“Kwa bahati mbaya sana kauli yangu ya ‘liwalo na liwe’ imetafsiriwa kwa namna tofauti. Hata dada yangu Halima Mdee nilimsikia akitilia shaka kauli hiyo na kuhusisha na tukio la kutekwa kwa Dk. Ulimboka.
“Nilichoaminisha ni kwamba hili jambo liko mahakamani, lakini tungetolea tamko la serikali bila kujali kwamba suala hilo liko mahakamani; ndiyo maana nikasema liwalo na liwe.’
Alisema baada ya mashauriano na wataalamu wa serikali jana usiku waliona si vyema kuendelea na tamko hilo hadi kesi iliyopo mahakamani itakapomalizika.
Kuhusu tukio la kutekwa, kupigwa kwa Ulimboka, Waziri Mkuu Pinda alisema serikali imeguswa na kushtushwa na tukio hilo, na akadai kuwa amesikitishwa na kuwepo kwa taarifa zinazoituhumu serikali kuhusika na unyama huo.
“Mazingira ya tukio hili bado yana utata mwingi, yanahitaji uchunguzi wa kina, kila mtu anasema lake, mwingine hili na wengine wanasema Serikali ndiyo imehusika,” alisema na kuongeza:
“Mimi nasema kama ni Serikali basi tutakuwa ni watu wa ajabu sana, Serikali tufanye ili iweje.”
Baada ya maelezo hayo, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Tundu Lisu, alimuuliza Pinda kwa nini asiwajibike katika suala la mgomo wa madaktari kwani ni yeye amekuwa akilishughulikia kwa muda na halionekani kupata ufumbuzi.
Baada ya swali hilo, Pinda alisema kuwa, yapo mazingira yanayoweza kumlazimu kuwajibika lakini siyo, haya ya mgomo wa madaktari kwani amejaribu kwa kiasi kikubwa kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.
“Yapo mazingira yanayoweza kunifanya nijiuzulu, lakini hili la madaktari nimejaribu kwa uwezo wangu, lakini be what it is (kwa jinsi lilivyo), kuna changamoto nyingi katika suala hili,” alisema Pinda.
Baada ya majibu hayo, Lisu alipewa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza na kusema “If you have tried your very best and you failed, why don’t you resign?” (kama umejaribu kufanya kila linalowezekana ukashindwa, kwa nini usijiuzulu??)
Baada ya swali hilo, Spika Anne Makinda alimtaka Waziri Mkuu kutojibu swali hilo la nyongeza kwa maelezo kuwa, linafanana na swali la msingi.
Hata baada ya maelezo ya Spika, Waziri Mkuu alijibu kwa kumueleza Lisu kuwa, anamuheshimu sana lakini lugha aliyotumia katika kuuliza swali lake siyo nzuri.
Mbunge Mwingine aliyezungumzia suala hilo ni Martha Mlata, aliyesema kuna uvumi kuwa, kuna watu wanawapa baadhi ya madaktari fedha ili wahamasishe wenzao kugoma.
Alisema kuwa, lengo la kikundi hicho ambacho hakukitaja, ni nchi isitawalike.
Akijibu swali hilo, Pinda alisema na wao (Serikali) wamesikia uvumi huo na wameviagiza vyombo vya usalama vilifanyie uchunguzi.

No comments:

Umesoma hizi hapa