Promote your business for free grow your business for life you don't need to spend more money anywhere.

THIS BLOG IS SPONSORED BY AHADIWAY ,ADVANTAGES FOR JOINING AHADIWAY BOON CAREER (ABC) CHAPTER = Employment opportunities within and outside the country. , Job experience , Self -employment , Field stations, part time jobs and chances to be trained.

Thursday, July 19, 2012

WEWE NI BORA JINSI ULIVYO,


WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO....ULEMAVU NI FIKRA ZAKO Pichani chini ni mwanariadha maarufu wa afrika ya kusini,Oscar Pistorius. Ni wakati mwingine wa kujitambua,sisi ni akina nani na tunakwenda wapi,na tunawezaje kwenda tuendako.....,Leo hii tukijadili kwa undani,uwezo tulionao,tusioutambua..Na mwisho tutatambua ya kuwa,ulemavu unaotambulika wa viungo,si kitu,bali ulemavu mkubwa ni wa kukosa kutumia uwezo wetu tulionao wa kufikiri na wa kuumba vitu vipya tukiifanya dunia kuwa sehemu bora,na kuishia kuishi kwa uoga na kulalamika,tukitegemea wengine kufikiri na kutenda kwa ajili yetu,tukiwa na macho,yasiyo upeo wa kuona,tukiwa na akili,na tusiitumie.......(huu ukiwa ni ulemavu mkubwa) SINA MIKONO,LAKINI HAIMAANISHI YA KUWA SINA UWEZO WA KUFIKIRI WALA KUTENDA (picha kwa hisani ya mtandao) Wewe ni kiumbe wa kipekee,uwe na miguu yote ,uwe umekosa miguu,ama mikono ,ama kiungo chochote cha mwili,bado unabaki kuwa kiumbe wa pekee aliyeumbwa,ukifanana na Muumba(asili yako) kwa uwezo wa kutenda na kuumba(wapo watakaohisi ya kuwa nafananisha mojakwa moja na Mungu,ni vema tukatambua ya kuwa Mungu anabaki kuwa Muumba kwa asili yake,na sisi tunabaki na ubora aliouumba,tukifanana na yeye aliye asili ya yote.....)hivyo uwezo wa binadamu kuyatawala mazingira yake haupo kwenye nguvu za mwili(misuli),haupo kwenye miguu,haupo kwenye mikono bali upo kwenye fikra zake. hivyo kwa kifupi,wewe ni bora jinsi ulivyo...uwe na miguu,uwe huna miguu,unabaki kuwa binadamu,unabaki kuwa kiumbe bora wa Mungu,...wewe ni bora jinsi ulivyo..... Kila tunapojitazama sisi,tusiishie kutazama sura tu,tusiishie kutazama rangi tu,tusiishie kutazama mvuto wa viungo vyetu,bali tujitazame ndani yetu ambako hutufanya tutambulike kwa wengine,kwani ndiko kunakoumba na kutufanya tuchague tutakuwa akina nani,tutaishi maisha yapi,na kutambua matokeo ya uchaguzi wetu kwa wengine... Yupo kijana mmoja,anaytambulika kwa jina la Nick Vujicic,aliyezaliwa akiwa hana mikono na akiwa na miguu mifupi sana,akizaliwa katika familia isiyo na uwezo mkubwa,alifika wakati akajitambua kuwa jinsi alivyo ni bora sana,akautambua uwezo wake ulio ndani mwake,akasoma na hata kumaliza chuo kikuu,akitenda mambo makubwa katika michezo,na hadi sasa ni mwenye mafanikio aliyoyakusudia,akitambua kuwa nuru ya maisha yake haionekani tu kwa sura yakebali kwa uwezo ulio ndani mwake...akitenda kwa ajili ya wengine....Huyu anatufunza ya kuwa ,sisis ni bora jinsi tulivyo...na tunastahili ushindi wowote kadiri ya uchaguzi wetu. NICK VUJICIC AKIWA KATIKA MOJA YA MICHEZO AIPENDAYO,WEWE NI BORA JINSI ULIVYO NINATAMBUA YA KUWA MIMI NI BORA JINSI NILIVYO,NIKICHAGUA MAISHA YANGU,NA NJIA YA KUISHI,NI KIYATIMIZA YOTE PASIPO KUJALI VIKWAZO VILIVYOPO,HATA PANAPOONEKANA HAPAWEZEKANI,MIMI NITAWEZAKWA KUWA NINAJUA NA KUTAMBUA KUWA MIMI NI BORA JINSI NILIVYO,NIKIWA NINA UWEZO MKUBWA NDANI MWANGU...NINAFURAHIA MAISHA YANGU,NIKIFURAHI,NIKICHAGUA MAISHA NA KUYAISHI...WEWE JE Hivyo basi,ulemavu ni tatizo la kifikra kuliko ilivyo kwamba,ulemavu ni kukosa viungo fulani vya mwili,hii ni tafsiri yangu ya kimtazamo....kama nlivyoandika katika makala iliyopita yenye kichwa cha habari..NI JINSI GANI TUNAPATA TUWAZACHO...Ni wakati sasa kuamka na kuondoa fikra zote za vikwazo ambavyo vinatufanya tusifanikiwe Ni wakati sasa wa kutambua kuwa sisi ni zaidi ya vile wengine wanavyotutazama,ama kudhani,na ni zaidi ya tunavyofikiri....sisi ni bora jinsi tulivyo na kila wakati tunapojitambua tunapata nafasi ya kuchagua maisha ambayo tunayapenda,tukiyaishi kwa furaha,na kuanzia sasa, hutasikiliza maneno ya wengine kuwa u mbaya,u kituko,ama hauvutii.....haya kwako si kitu,kwani wewe ni bora ukiwa na uwezo wa kuchagua na kuyaishi maisha yenye furaha..na hayo ndiyo mafanikio NIKIJITAMBUA,NITATAMBUA UWERZO WANGU ,NITAWEZA KUCHAGUA MAISHA YANGU NA KUYAFIKIA MAFANIKIO AHSANTENI SANA, PONGU 

No comments:

Umesoma hizi hapa