Promote your business for free grow your business for life you don't need to spend more money anywhere.

THIS BLOG IS SPONSORED BY AHADIWAY ,ADVANTAGES FOR JOINING AHADIWAY BOON CAREER (ABC) CHAPTER = Employment opportunities within and outside the country. , Job experience , Self -employment , Field stations, part time jobs and chances to be trained.

Monday, November 8, 2010

KIKWETE AAPISHWA URAIS WA TANZANIA

MGABE,KIBAKI,KABILA,MKAPA,LOWASA WAHUDHURIA, KARUME,SEIF SHARIFU WASHINDWA KUIMBA WIMBO WA TAIFA LA TANZANIA!!

RAIS Jakaya Kikwete baada ya kuapishwa kuwa rais kwa kipindi cha miaka mitano ya awamu ya pili
DR.Wilbroad Slaa aliyewania urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, hajatokea katika sherehe za kuapishwa rais kikwete
Rais Mstaafu wa awamu ya sita ya serikali ya mapinduzi Zanzibar, huiyu ndiye aliyewezesha kwa kiasi kikubwa kuundwa kwa serikali ya mseto Zanzibar
Rais wa jamhuri ya watu wa Kenya Mwai Kibaki amehudhuria sherehe za kuapishwa jk
RAIS wa jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo Joseph Kabila akisalimiana na JK, Kabila amehudhuria sherehe za kuapishwa kwa jk katika uwanja wa uhuru
 katibu mkuu wa chama cha wananchi cuf na makamu wa rais mtarajiwa wa Zanzibar Seif Hamad Sharifu amehudhuria sherehe za kuapishwa kwa jk
rais jk akikagua vikosi vya ulinzi na usalama vilivyotoa gwaride la heshima wakati wa sherehe za kuapishwa kwake
rais wa zimbabwe Robert Mugabe amehudhuria pia kuapishwa kwa jk Dar es salam
RAIS JAKAYA KIKWETE ameapishwa jkuiongoza jamhuri ya muungano wa Tanzania katika kipindi cha pili cha miaka mitano baada ya kutangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi kuwa mshindi wa nafasi hiyo kwa asilimia 61.1 dhdi ya wagombea wengine sita wa urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini kote okt 31 mwaka huui

Kikwete ambaye ameibuka na ushindi huo pungufu kwa asilimia 20.1 ya ushindi wake wa kimbuka wakati alipoingia kwa mara ya kwanza katika nafasi hiyo mwaka 2005 amefuatiwa na mgombea wa chama cha CHADEMA dr. Wilbroad Silaa ambaye amegoma kuyatambua matokeo hayo kwa madai kuwa yalichakachuliwa. Dr. Slaa hakuhudhuria katika sherehe za kuapishwa kwa KIkwete, na hata wakati wa kutangazwa kwa matokeo hayo pale katika viwanja vya Karimjee pia hakutokea,Mshindi wa tatu ambaye ni Ibrahimu Haruna Lipumba alihudhuria wakati wa utangazwaji wa matokeo na hata wakati wa sherehe za kuapishwa jk ameonekana.

Hata hivyo profesa Lipumba aliyechukua nafasi ya dr. Slaa katika hotuba fupi ya kushukuru kwa niaba ya wagombea walioshiriki katika uchaguzi huo aliitupia lawama tume ya taifa ya uchaguzi kwa kushindwa kuhamasisha watu waliojianmdikisha kuweza kupiga kura, na pia aliwalaumu kwa kasoro nyingi zilizojitokeza wakati wa zoezi la upigaji kura na kuitaka tume hiyo kujisafisha na kujirekebisha ili chaguzi za Tanzania ziweze kuwa huru na haki.

Katika sherehe za leo, zimehuidhuriwa na watu mbalimbali maarufu wakiwemo marais ,mabalozi wa nchi mbalimbali barani Afrika,

Hata hivyo cha kuchekesha sijui kwa kutojua au laa! katibu mkuu wa cuf maalimu Seif Sharifu  na rais mstaafu wa serikali ya Zanzibra dr. Aman Karume hawakuweza kuimba wimbo wa taifa wa Tanzania wakati ukipigwa nyakati zote ulipopigwa katika sherehe hizo hali iliyoibua maswali kutoka kwa wafuatiliaji wa mambo ya siasa na waliokuwa wakifuatilia sherehe hizo.!

Hata hivyo miongoni mwa watu waliokuwa wakifuatilia walijipa majibu wenyewe kuwa pengine hawakujisikia kuuimba au laa,lakini hali ilikuwa tofauti kwa rais wa awamu ya saba wa Zanzibar dr. Ally Mohamed Shein aliyeonekana akiuimba wimbo huo kwa ufasaha sawa na rais Jk na watanzania wengine

No comments:

Umesoma hizi hapa