Promote your business for free grow your business for life you don't need to spend more money anywhere.

THIS BLOG IS SPONSORED BY AHADIWAY ,ADVANTAGES FOR JOINING AHADIWAY BOON CAREER (ABC) CHAPTER = Employment opportunities within and outside the country. , Job experience , Self -employment , Field stations, part time jobs and chances to be trained.

Tuesday, October 19, 2010

Viongozi waache kujipendelea katika utoaji mikopo.

Utete,Wilaya ya Rufiji,Mkoa wa Pwani
RAIS  Jakaya Mrisho Kikwete na Mgombea Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) amewataka viongozi wa umma kuacha kujipendelea wenyewe katika kutoa huduma ukiwamo upatikanaji wa mikopo ya wajasiriamali ama matrekta.‘Mikopo hii ni ya wajasiriamali tunaitoa kwa ajili ya watu masikini wasiokuwa na kipato kikubwa na wasiokuwa na fursa ya kupata mikopo kwingine popote. Hii siyo mikopo ya viongozi. Siyo mikopo ya viongozi kujikopesha wenyewe,” Rais Kikwete ameuambia mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mjini Utete, Wilaya ya Rufiji, Mkoa wa Pwani.Rais Kikwete amerudia wito huo wakati alipohutubia mamia kwa mamia ya wakazi wa Kilwa Masoko, Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi, katika mkutano mwingine uliofanyika jioni ya leo, Jumatatu, Oktoba 18, 2019 kwenye Bustani ya Mkapa.Akisisitiza umuhimu wa kuwakopesha wananchi matrekta makubwa na madogo kwa namna ya haki, Rais Kikwete amewambia wananchi hao:“Matrekta haya hayakukusudiwa nyie maofisa. Haya ni kwa ajili ya kuwakopesha watu wa kawaida katika jitihada za Serikali kuwainua watu kutoka kwenye umasikini.”Rais Kikwete amewataka wagombea udiwani kupitia CCM kuhakikisha kuwa wananarekebisha hali hiyo baada ya Uchaguzi Mkuu, na kuhakikisha kuwa mikopo na matreka hayo yanatolewa kwa haki bila maofisa kujipendelea wenyewe.“Kazi yetu sisi viongozi ni kulinda haki na maslahi ya wananchi. Tusifanye kazi ya kutetea maslahi ya watu wachache. Tuko hapa kusimamia maslahi ya wengi na hii ndiyo kazi ambayo chama chetu kimekuwa kifanya tokea TANU na hadi CCM.”
Rais Kikwete leo amefanya mikutano ya kampeni katika maeneo ya Kimanzichana na Utete katika Mkoa wa Pwani, na Kilwa Masoko, Mkoa wa Lindi.

No comments:

Umesoma hizi hapa