Promote your business for free grow your business for life you don't need to spend more money anywhere.

THIS BLOG IS SPONSORED BY AHADIWAY ,ADVANTAGES FOR JOINING AHADIWAY BOON CAREER (ABC) CHAPTER = Employment opportunities within and outside the country. , Job experience , Self -employment , Field stations, part time jobs and chances to be trained.

Thursday, September 23, 2010Jinsi ya kupata mwenza ukiwa ughaibuni(ulaya)


HAYA, leo hebu tuangalie jinsi unavyoweza kupata mwenza wa kuishi naye ukiwa uko ughaibuni. Njia ya kwanza ni kupitia njia ya mtandao, ndiyo eeh kwenye mtandao au internet unaingia chat room, una chat wee, mpaka iko siku kinaeleweka. 
Lakini, kwa njia hii wako waliofanikiwa nao wako waliolia pia. Ni kama kucheza kamari vile maana kwenye mtandao nyie mnachat, mnatumiana picha, mnaongea mnapatana, na mara nyingi huanza kama marafiki wa kawaida tu. Naweza kusema marafiki wa kalamu enzi zetu! Mnaendelea kujenga urafiki mpaka mnafika mahali ukikosa kuchat siku moja tu unakuwa mgonjwa! Ndio dalili zenyewe hizo! Sio za malaria! Hapana za ka ule kaugonjwa!
Sasa hapo mtandelea kuchat kama marafiki wa kawaida, mwisho mnaandikiana barua pepe ndeefu, kisha mnapeana majina yenu ya ukweli na kutamkiana yale yaliyowasibu moyoni! Hiyo ni njia mojawapo.
Nyingine ni kupitia magazeti ya mtandao au kwenye mitandao mbali mbali utakuta mtu anatafuta mwenza wa kuishi naye. Hapa hakuna haja ya kuogopa, kwa sababu kwa mazingira ya sasa utakuta msichana pengine yuko Khazastan anasoma, na vijana alio nao huko wote wana wenyewe, sasa inabidi tu ajitangaze kwenye mtandao kuwa anatafuta mwenza wa kuishi nae. Hakuna ubaya wala tatizo lolote kwa mwanamke kufanya hivyo ingawa kutokana na makuzi na malezi yetu wengine wanaweza kumuelewa vibaya au wakaona kuwa hafai.
Lakini ni msichana jasiri huyu, hataki kuendelea kupoteza muda wala kusononesha roho yake kwa kuwa tu anaogopa kuwaambia watu kuwa jamani eeh na mie nahitaji mwenza, nahitaji kuwa mapenzini. Na hata walio hapa hapa nyumbani wanaweza kuwapata wenza wa kuishi nao kwa kupitia mitandao, kusoma matangazo ya kwenye magazeti mbali mbali iliyo na safu ya wanaotafuta marafiki au wachumba!
Jambo la msingi ni kuwa muwazi tangu mwanzo unataka nini kutoka kwa huyo rafiki au mchumba unayemtafuta. Unatakiwa useme vigezo unavyovitaka ambavyo vimejijenga ndani ya fikra zako kuwa nataka mwanaume au mwanamke wa umri fulani, mwenye urefu kiasi fulani, ├║seme na rangi kabisa, usije yakakuta yale ya kijana wangu aliyekuja kunilalamikia wamemchagulia mchumba wa rangi asiyetaka! Ndiye yale yale niliyosema ya ubaguzi wa rangi, lakini mapenzi bwana yana kitu cha ajabu kabisa, wakati mwingine vigezo vyoote ulivyoviweka unaweza kuviweka kando ukimpata aliyeugusa moyo wako ukagusika!
Cha msingi ni kutaka picha za angle tofauti, si unajua tena, upande, mbele, nyuma, akiwa na make up, bila make up. Na kina dada waambie hao wakaka wawatumie picha zao walizopiga siku za karibuni tena wote nawaasa msiombe picha zinazopigwa kwenye sherehe kama za harusi sijui nini, mwambie akuonyeshe kama ni mwanaume au mwanamke jinsi alivyo. Nilishagusia huko nyuma kuna mtu kamgharamia msichana masomo wee, mpaka kamaliza, ndoa ikafungwa akatumiwa nauli, kufika Airport msichana hataki kwenda na mume, anasema siye huyu mume wangu anatoa picha aliyoletewa, haifanani na ya mume, kumbe yule bwana alituma picha yake ya zamani enzi zake zilipendwa!!
Njia nyingine kwa watu walio mbali au ughaibuni wanaweza kutumia ndugu na jamaa kama nilivyosema katika makala zilizopita ila sasa inabidi uwe makini kweli kweli. Lazima uwaambie hao jamaa zako chagua lako, uwape vigezo vyako ili wakutafutie kulingana na unavyotaka. Lakini hiyo unakuwa unawapa kaazi kweli kweli mimi nionavyo huu urembo wa nje mara nyingi huwa hauna uzito sana cha msingi ni tabia tu ya mtu maana wakati mwingine huo unakuwa uzuri wa mkakasi kumbe ndani kipande cha mti! Nitahitimisha Jumanne ijayo.
Ukiwa na maoni, au maswali niandikie parua pepe kwa kutumia anuani hiyo hii;

No comments:

Umesoma hizi hapa