MWIGIZAJI wa kike wa filamu na muziki Bongo zuwena Mohamed ‘Shilole’ amemtangazia hali ya hatari msanii mwenzake wa filamu na mtangazaji wa televisheni Christina John ‘ Sintah’ kuwa popote atakapomkuta lazima amchape kwa kipigo ambacho hatasahau katika maisha yake, Shilole kaongea hayo kufuatia kuandikwa na mwanadada huyo katika mtandao wake akimbeza kwa kejeli.
“Ni kweli sisi wanawake hatupendani na kuwa na wivu wa kijinga, mtu anakurupuka anakotoka bila hata kufanya utafiti na kunibeza eti sina uwezo wa kuimba na JLO (Jenifer Lopez) kuna mtu aliyetegemea mimi kwenda kufanya show Marekeni! Sasa ninachomwambia ninamtafuta nikikutana naye nimtapa kipigo cha Mbwa mwizi,”aliongea kwa hasira Shilole.
Katika mtandao wake Sintah aliandika kwa kusema Shilole ni sawa na mtu anayeota ndoto za mchana, na kumkejeli kwa kusema kuwa aendelee kuota anaweza baadae kurudi katika hali yake, sehemu ya maneno yanayomkera Shilole ni haya
“Shilole bwana hii week katujia na kali kuliko eti ameongea na Benny Medina (Jlo’s Manager) ili aweze kufanya collabo na my sister, heee yes inawezekana maana hakuna lisilowezekana chini ya jua lakini swali ni?? wataimbaje?? yule dada yake na mie ni RnB na music wa Shilole bado sijaujua ni chakacha ama nini sasa naomba msaada kwenye tuta wadau wa music, hili linauwezekano??,”
“ Chakacha na RnB?? Kwa sababu Shilole nyimbo zake sawa na Snura wa majanga, kidogo Linah angeniambia ana collabo na my sisy ningeelewa sasa Shilole?? Ndoto za mchana ila si vibaya kuota maana ukishtuka unarudi ktk reality,”
Shilole anasema kuwa hajawahi kumuona mwanamke mwenye roho dhaifu kama Sintah, anajifanya anambabaikia Jlo wakati hata hajulikani, ameshangaa watu wa Bongo kuwa na tabia ya kudharau muziki wa nyumbani na kubabaikia muziki wa Marekani wakati wenyewe hawana muda muziki wa hapa Bongo, anamchukia Sintah kwa kuongea kitu asichojua na kumponda yeye na Snura.
“Mimi sikuwa nimeenda Marekani kwa ajili ya kuomba kumshirikisha J-lo kuimba naye lakini baada ya meneja wake kuja kuniona na kumpelekea video za muziki wangu alikubali kufanya kazi na mimi, ilitakiwa nionane naye siku ya Jumapili lakini ndio siku niliyoondoka na ninarudi huko kwa ajili ya kazi hiyo, sijui nikifanya naye kazi atajificha wapi?,” anasema Shilole.
Shilole anasema Mungu ni mkubwa hata kama kuna mtu anayemchukia kwa mafanikio yake bado Mungu ana nafasi kubwa kuwazima watu wenye roho mbaya wivu kama Sintah ambaye anaonekana yupo tayari kwa ajili ya kuwaombea matatizo watu wanaojituma kwa ajili ya kuendesha maisha yao.
Read more: http://talkbongo.blogspot.co.uk/2013/07/shilole-aapa-kumchapa-makonde-sintah.html#ixzz2ZrGD9r7n

No comments:
Post a Comment