MWANAMKE mmoja mkazi wa Kijiji cha Kasumuru, Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya,
Grace Joel Lwesha (19), amelia baada ya kujifungua watoto walioungana.Akizungumza
na waandishi wetu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jengo la Watoto, Grace
alilia kutokana na kile alichodai kujifungua watoto walioungana wakati yeye
ni maskini. Watoto hao mapacha wa kiume, Eliudi na Elikana wameungana
sehemu ya makalio hivyo kulazimika kutumia sehemu moja ya haja kubwa.
Grace aliwaambia waandishi wetu kwamba, watoto hao walizaliwa katika
Hospitali ya Kyela, Februari 20, mwaka huu wakiwa na miguu miwili na
mikono miwili kila mmoja.
“Baada ya kujifungua Machi mosi nilihamishiwa katika Hospitali ya
“Baada ya kujifungua Machi mosi nilihamishiwa katika Hospitali ya
Mkoa wa Mbeya kwa uchunguzi zaidi ili waweze kujua ni jinsi
gani watakavyotenganishwa,” alisema.
Hata hivyo, hospitali hiyo ya mkoa haikufanikiwa badala yake Machi 16,
Hata hivyo, hospitali hiyo ya mkoa haikufanikiwa badala yake Machi 16,
walimhamishia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo kuanzia
hapo mpaka sasa anafanyiwa maandalizi kwa ajili ya safari ya kupelekwa
nchini India kwa upasuaji.
“Ninawapenda sana watoto wangu hawa pamoja na kwamba wapo
“Ninawapenda sana watoto wangu hawa pamoja na kwamba wapo
katika hali hii, ndugu zangu walipokuja hospitalini kuniona akiwema
mama yangu walinifariji na kunisihi nisiwachukie nizidi kuwapenda.
“Kuwatunza ni kazi ngumu sana kwani mara nyingi wamekuwa
“Kuwatunza ni kazi ngumu sana kwani mara nyingi wamekuwa
wakininyima usingizi kwa sababu wamekuwa wakilala kwa nyakati tofauti.
“Nakumbuka siku niliyojifungua mume wangu alikosa raha lakini sasa
“Nakumbuka siku niliyojifungua mume wangu alikosa raha lakini sasa
anawapenda kwani amejua kuwa hii ni zawadi kutoka kwa Mungu.
“Maisha yetu ni magumu kwani tunatoka kwenye familia maskini,
kazi yetu ni kilimo cha kutumia jembe la mkono hivyo bado kuna mahitaji
mengi nashindwa kumudu. Nichukue nafasi hii kuwaomba msaada
Watanzania wote walioguswa na tukio hili,” alisema Grace.
Grace alifunga ndoa na Erick William Mwakyusa Desemba 23, 2010 na
Grace alifunga ndoa na Erick William Mwakyusa Desemba 23, 2010 na
katika ndoa yao wamejaliwa kupata mtoto mmoja aitwaye Lide (3) na hao
mapacha ni uzao wake wa pili.
Mama huyo anaomba msaada kwa mtu yeyote aliyeguswa na habari hii
Mama huyo anaomba msaada kwa mtu yeyote aliyeguswa na habari hii
atume mchango wake kupitia namba 0753308525 ambayo ni ya
mumewe au aende kumuona Muhimbili.
No comments:
Post a Comment