Na Waandishi Wetu JIJI la Dar es Salaam wiki iliyopita lilikumbwa na
matukio ya kutisha yaliyosababisha lionekane ni la damu baada ya majambazi kufanya uhalifu
wa kutisha sehemu mbalimbali kwa kuwapiga risasi watu huku wakipora
fedha na mali.
Zwahili Miraji.
Gazeti hili lilipita maeneo mengi na kubaini yafuatayo:DENTI CHUO KIKUU ALIVYOMIMINIWA RISASI
Lilikuwa ni kundi la majambazi sita waliovamia Chuo Kikuu cha Dar es salaam
usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita na kufanikiwa kuwapora wanafunzi
waliokuwa wakijisomea vitu kadhaa na kummiminia risasi mmoja wao.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa 9.00 usiku katika ukumbi ujulikanao
kwa jina la Yombo 1 ambapo mwanafunzi Alex Robert, 26, alipigwa risasi.
Kwa mujibu wa taarifa za kiuchunguzi, majambazi waliingia katika ukumb
i huo wakiwa na silaha za jadi pamoja na bunduki aina ya shortgun.
Chanzo makini cha gazeti hili chuoni hapo kilisema kuwa
majambazi hayo yalipofika ukumbini yaliwaamuru wanafunzi hao kulala
chini na kukabidhi kila walichokuwa nacho, amri ambayo wanafunzi hao
walitii kwa kuwapa kompyuta mpakato, simu na fedha.
Hata hivyo, mwanafunzi mmoja aliamka na kuwaomba wamrejeshee flashi
yake, ambapo jambazi mmoja aliichomoa na kumtupia ndipo Alex
alipoomba kurudishiwa kitambulisho kwa madai kuwa asingeweza
kuingia ndani ya chumba cha mtihani bila kuwanacho.
Kitendo cha kuomba kitambulisho ndiyo chanzo cha kupigwa risasi mwanafunzi huyo
wa kitivo cha sheria.
Mwanafunzi huyo alipigwa risasi mbele ya wenzake Joseph Hansi, Lunura Masalu
na Kitojo Karani na baada ya tukio hilo wanafunzi hao walimchukua mwenzao na
kumpeleka kituo cha afya chuoni hapo na baadaye alikimbizwa katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Mara baada ya kitendo hicho, baadhi ya wanafunzi waliandamana kuelekea Kituo
cha Polisi Chuo Kikuu kutaka msaada zaidi baada ya kuona askari walioajiriwa na
chuo hawakutokea kupambana na wahalifu hao.
Wanafunzi waliliambia gazeti hili kuwa kwa hivi sasa usalama wa maisha na mali
zao unatia shaka kutokana na askari wa chuo kutowajibika ipasavyo.
“Siku ya tukio Ukumbi wa Yombo 1 haukuwa na mlinzi yeyote hadi
tulipoomba msaada kutoka polisi makao makuu, huu ni uzembe,
” alisema mwanafunzi mmoja kwa sharti la kutotajwa jina gazetini.
Makamu Mkuu wa Chuo,Utawala, Yunus Mgaya aliliambia gazeti
hili kuwa uongozi wa chuo hicho unasikitishwa na tukio hilo na
akaahidi kuimarisha ulinzi.
Afisa Habari Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Aminieli
Aligaeshi alisema mwanafunzi huyo amefanyiwa upasuaji na
kutolewa risasi tumboni na hivi sasa yuko chini ya uangalizi wa
madaktari katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman
Kova amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na akasema majambazi
hayo yalikuwa na silaha ikiwemo bunduki na upelelezi unaendelea.
Akizungumzia maandamano yaliyotokea chuoni hapo alisema:
“Wanafunzi chuoni hapo walikuwa na lengo la kushinikiza ulinzi.
Jeshi la polisi kanda maalum kwa kushirikiana na makamanda
wa mikoa wanaendelea na msako mkali dhidi ya wahalifu hao.”
MFANYABIASHARA APIGWA RISASI, APORWA
Wakati huohuo, Ijumaa iliyopita saa 8 mchana majambazi yakiwa
na pikipiki na bastola yalimpiga risasi na kumpora kiasi kikubwa
cha fedha wakala wa magazeti ya makampuni mbalimbali nchini.
Wakala huyo aliyejulikana kwa jina la Zwahili Miraji Mrutu akizungumza
na gazeti hili akiwa Hospitali ya Muhimbili alisema, alikuwa maeneo ya
mitaa ya Kipata na Swahili jijini Dar akiwa anapeleka fedha benki ghafla
alijikuta akipigwa risasi kifuani na kuporwa pesa.
Akizungumza kwa shida katika Wodi ya Kibasila, Mrutu alisema:
“Majambazi hayo yalikuwa na pikipiki na wakaniambia niwape fedha
, nilipozing’ang’ania, walinipiga risasi moja kifuani na mbili hewani
kwa lengo la kutawanya watu.”
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, ACP Marietha Minangi
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Tukio hilo kweli limetokea na majeruhi huyo yupo katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili akiendelea na matibabu huku nasi tukiendelea
na upelelezi,” alisema Kamanda Minangi.
ANYONGWA KIKATILI
Naye mwendesha pikipiki ya miguu mitatu maarufu kama Bajaj amb
aye kituo chake kilikuwa maeneo ya Sayansi, Beatus Kisanga, mkazi
wa Makumbusho, Dar, ameuawa kinyama kwa kunyongwa na kamba
na majambazi.
Tukio hilo lilitokea ndani ya Baa ya Serengeti iliyopo maeneo hayo
huku kaka yake ambaye ni mlinzi wa baa hiyo aitwaye Batlista Kisanga
alikutwa akiwa hoi hajitambui.
Akizungumza na Uwazi, mmiliki wa baa hiyo, Venancy Lyimo alisema
kuwa marehemu aliuawa saa 11 alfajiri naye alipewa taarifa hizo kwa
njia ya simu na kijana ambaye anafanya usafi mishale ya saa moja asubuhi.
“Kijana huyo aliniambia kuwa alimkuta mlinzi akiwa kaunta hajitambui
huku vinywaji vikiwa vimetolewa nje na kuzagaa chini. Nilitoka nyumbani
kuja hapa kazini,” alisema.
Aliongeza kuwa baada ya kufika alimkuta marehemu akiwa amefungwa
kamba mikononi na miguuni huku mdomoni amefungwa kitambaa na
mwili wake ukiwa umetupwa kwenye jiko la kuchomea nyama.
“Kinachoonekana ni kwamba wale majambazi waliwapa sumu hawa jamaa
,’’ alisema Lyimo.
Aliongeza kuwa, aliwapigia simu polisi waliofika na kuuchukua mwili wa
marehemu huku mlinzi akipelekwa Hospitali ya Mwananyamala kwa
matibabu.
Kaka wa marehemu aitwaye Yesse Peter akizungumza na Uwazi, alisema
kwamba mwili wa marehemu ungesafirishwa wakati wowote kwenda
Mbeya kwa mazishi.
KACHERO WA POLISI ANUSURIKA KUUAWA
Wakati hayo yakitokea, askari wa upelelezi aliyefahamika kwa jina la
Samwel Michael usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita alinusurika
kuuawa na wananchi waliomhisi kuwa ni jambazi baada ya kupata
ajali ya bodaboda.
Askari huyo alihisiwa na wananchi kuwa ni muhalifu baada ya kukutwa
na bastola huku akiwa amepoteza fahamu.
Tukio hilo lilitokea karibu na Kituo cha Drive Inn, Msasani jijini Dar
ambapo mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema: “Nilianza kupata
mashaka baada ya kumuona jamaa akiendesha pikipiki aina ya Bajaj
Boxer kwa kasi.
“Nikiwa namshangaa ghafla nilimuona akilivaa hili greda ambalo
limeegeshwa hapa baada ya kumaliza kufanya ukarabati wa hii barabara.”
Akiwa eneo la tukio mwandishi wetu alimshuhudia askari huyo akitapatapa
kutaka kuamka huku baadhi ya wananchi wakisema huenda ni
jambazi na kutaka kummaliza.
Wakati wananchi hao wakitaka kummaliza ghafla alitokea askari wa
kikosi cha usalama barabarani na kuchukua bastola iliyokuwa
pembeni ya majeruhi huyo na kuanza kumpekua.
Baada ya kumkagua alimkuta na kitambulisho chake cha kupigia
kura pamoja na cha kazi kilichoonesha alikuwa askari wa upelelezi
pia alimkuta na pingu pamoja na nyaraka zingine.
Baada ya kupata vielelezo hivyo afande huyo aliwaondoa hofu wananchi
waliokuwa wakitaka kummaliza majeruhi huyo na kuwaambia kuwa
alikuwa ni askari wa upepelezi aliyekuwa kazini.
Baada ya kutulizwa wananchi hao waligeuka wasamaria wema na kuanza
kumsaidia majeruhi huyo mpaka walipofika askari wengine ambao
walimuwahisha hospitali kupata matibabu.
No comments:
Post a Comment