Awali Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), alibadilisha mashtaka na Lulu kutuhumiwa kuua bila kukusudia.
Kutokana na mabadiliko hayo sasa Lulu ameepuka adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa tuhuma za kumuua aliyekuwa msanii maarufu nchini, Steven Kanumba.
Sasa Lulu endapo atapatikana na hatia, adhabu yake itakuwa ni kifungo cha maisha au kuachiwa huru.
Hali hiyo inatokana na kifungu cha 196 cha kanuni za adhabu ya kosa la kuua bila kukusudia na anayepatikana na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha, miaka kadhaa au kuachiwa huru.
No comments:
Post a Comment