KUJISTIRI ndio hasa lengo la awali la uvaaji. Na kupendeza ni jambo la pili ambalo limekuwa likizingatiwa sana na wanawake. Lakini ili haya yote yafikiwe, zipo dondoo maalumu ambazo endapo zikitumiwa vyema azma zote mbili hufanikiwa.
Kwa mujibu wa wataalamu wa mitindo ya mavazi, dondoo za mavazi hutofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Na hii husababishwa na tofauti ya maumbo iliyopo baina yao. Katika kipindi kilichopita tulijaribu kuangalia dondoo muhimu za mavazi kwa wanawake wanene, wembamba na wafupi. Je ungependa kufahamu dondoo za uvaaji kwa wanawake warefu?
Soma hapa upate baadhi ya dondoo muhimu za mavazi kwa wanawake warefu wembamba.
Suruali
Wanawake warefu wamekuwa wakikabiliwa na tatizo kubwa la kupata mavazi yanayowatosha kulingana urefu wao. Hivyo wakati mwingine huishia kwa mafundi wa kushona kwa ajili ya kuongezewa urefu wa nguo zao.
Ikiwa hili la kuongeza halitafanikiwa, achana na hiyo nguo.Usivae 'njiwa' kwani pamoja na kukufanya uonekane kama umeazima , pia itakufanya uonekane mrefu zaidi kuliko umbo lako halisi.
Msaada mwingine ni kwamba unapokwenda kununua suruali, hakikisha unachagua ile yenye urefu wa ziada. Wakati mwingine ni bora kununua surali ndefu kwani itakuwia rahisi endapo utaamua kupunguza.Suruali zenye mifuko ama zenye marinda zina uwezo mkubwa wa kukuongezea 'shape'. Hivyo hupendeza zaidi ikiwa ndio litakuwa chaguo sahihi kwa wanawake hawa.
Blauzi
Kama wewe ni mrefu mwembamba na huna maziwa makubwa, jaribu kutengeneza umbo la kike kwa kutumia mavazi yako. Tumia blauzi zenye mapambo ya mikunjo mikunjo sehemu ya kifuani.
Ikiwa hutapendelea hili, unaweza kutumia sidiria zenye sponji ili kunyanyua kifua chako na kuboresha muonekano wako. Blauzi fupi fupi ndio hasa chaguo lako sahihi.
Sketi
Pamoja na kuwa wengi wao hupendelea kuvaa sketi za kubana, lakini sketi za puto, bwebwe ama zile za marinda ndio hasa sahihi kwa wanawake warefu wembamba.
Mara nyingi hupendeza zaidi ikiwa sketi hizi zitakuwa fupi. Kwani huonyesha vizuri miguu ya mhusika na hivyo kudhihirisha urembo wake wa asili.
Ikiwa mvaaji atachanganya sketi yake na blauzi fupi ya chiffon au silk na kujipamba na bangili, ataonekana mwenye mvuto wa kipekee.
Viatu
Viatu virefu vina uwezo mkubwa wa kukufanya uonekane mrembo zaidi. Hivyo katika hili una uhuru wa kuchagua uvae viatu gani kulingana na wakati na mahali unapotaka kwenda.
Wengi hudhani kuwa kuvaa viatu virefu kutawafanya wawe warefu zaidi na hivyo kuchusha. Lakini ukweli ni kwamba vaa kile kinachokuweka huru zaidi.
Mkanda
Wakati mwingine hupendeza zaidi ikiwa utatumia mkanda kama kiunganishi cha mavazi yako. Tumia mkanda kunakshi tops, cardigan au hata makoti. Kwani utasaidia kwa kiasi kikubwa kugawa mwili wako kwa sehemu ya juu na ya chini.
Ikiwa utapendelea kutumia mkanda kwenye mavazi yako, unashauriwa kutumia rangi zinazoonekena kwa urahisi. Na kama si mpenzi wa mkanda unashauriwa kuvaa blauzi fupi fupi, hii itaifanya miguu yako ionekane vizuri na kwa urahisi.

No comments:
Post a Comment