Promote your business for free grow your business for life you don't need to spend more money anywhere.

THIS BLOG IS SPONSORED BY AHADIWAY ,ADVANTAGES FOR JOINING AHADIWAY BOON CAREER (ABC) CHAPTER = Employment opportunities within and outside the country. , Job experience , Self -employment , Field stations, part time jobs and chances to be trained.

Saturday, May 26, 2012

Kuvuta moshi wa sigara inayotumiwa na mtu mwingine

Kuvuta moshi unaotokana na mtu mwingine au vitu vingine ambao sio moja kwa moja.ni hali ya kuvuta hewa ya moshi unaotokana na mtu anayevuta sigara au mazingira ya moshi wa tumbaku (ETS), kutoka kwa bidhaa za tumbaku inayotumiwa na watu wengine. Hutokea wakati moshi wa tumbaku unaenea mazingira yoyote na kusababisha athari ya kuvuta hewa kwa watu wanaoishi hapo. Ushahidi wa kisayansi unaonyesha kwamba kuvuta hewa ya moshi utokanao na mtu anayevuta tumbaku husababisha ugonjwa, ulemavu, na kifo.
Kuvuta moshi wa sigara inayotumiwa na mtu mwingine kumechangia pakubwa katika mjadala juu ya madhara na udhibiti wa bidhaa za tumbaku. Tangu mapema miaka ya 1970, sekta ya tumbaku imekuwa na wasiwasi kuhusu kuvuti moshi wa sigara inayotumiwa na mtu mwingine kama tishio kubwa kwa maslahi ya biashara yake, [10] madhara kwa walioko ambao hawavuti sigara', Ilionekana kama shinikizo kuu la kudhibiti bidhaa za tumbaku. Licha ya ufahamu wa mapema kwa uwezekano wa madhara ya moshi wa sigara inayovutwa na mtu mwingine,sekta ya tumbaku iliratibu uhandisi wa pambano la kisayansi kwa lengo la kuchunga udhibiti wa bidhaa zao. Hivi sasa, hatari za kiafya za moshi wa sigara ni suala la makubaliano ya kisayansi, na hizi hatari zimekuwa moja ya motisha kubwa kwa ajili ya kupiga marufuku kuvuta sigara katika maeneo ya kazi na dani ya maeneo ya umma, ikiwa ni pamoja na mikahawa, bar na klabu za usiku.

No comments:

Umesoma hizi hapa