Team ya "Saidia Gongo La Mboto - UK" kazini
Jumuiya ya wafanyakazi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) wakikabidhi msaada wao
Wito umetolewa kwa jamii kuendelea kujitokeza zaidi kuchangia waathirika wa milipuko ya mabomu iliyotokea katika kambi ya JWTZ Gongolamboto.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na jumuiya ya wafanyakazi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) leo jijini Dar es salaam kaimu mkuu wa chuo hicho na Mkurugenzi wa Mafunzo Bw. Athman Ahmed amesema jamii ya watanzania bila kujali eneo wanalotoka wanao wajibu wa kutoa misaada mbalimbali pindi majanga mbalimbali yanapotokea nchini.
Amesema Jumuiya ya wafanyakazi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kwa kutambua ukubwa wa tatizo na hali halisi ya mahitaji ya waathirika wa mabomu wameamua kuchangia msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo mchele , sukari , chumvi na mahitaji mengine yenye thamani ya jumla ya shilingi milioni moja.
“ Menejimenti kwa niaba ya chuo tumeguswa sana kutokana na wenzetu kuathirika na milipuko ya mabomu na kuamua kujitoa kwa vitu tulivyonavyo tukiwa kama sehemu ya jamii kwa kutambua mchango wetu na wajibu wetu kwa waathirika” amesema.
Kwa upande wake Afisa tarafa wa Ukonga Bw.Jeremiah Makolele ambaye amepokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na mwenyekiti wa kamati ya maafa amewashukuru wafanyakazi wa chuo hicho kwa moyo waliouonyesha wa kuchangia waathirika wa milipuko ya mabomu na kutoa wito kwa wananchi zaidi kuitokeza kuchangia.
No comments:
Post a Comment