' ndio maana malaya wewe'
'peleka huko kazi yako si kujiuza tu'
'wewe hujatualia ni mapepe tuu'
'we unazani nisinge kuoa ungeolewa wewe?'
hayo ni baadhi ya maneno ambayo nimewasikia baadhi wa wanawake wenzangu wakilalamikia wanaume zao kuwatukana hivyo,kwa kweli akina baba haipendezi kumwambia mwanamke aliyekuzalia watoto malaya hata kama amekukosea!maneno mengine huwa hayafutiki moyoni haraka na yanapunguza mapenzi kwa kiasi kikubwa sana. Tujaribu kugombana kwa kutukia akili ni sio mioyo, tujaribu kutumia kauli ambazo zitajenga uhusiano na sio kubomoa ni hayo tu.
Angalizo; wapo pia wanawake wenye midomo michafu sana kwa wanaume au wapenzi wao hili pia laweza kuwa ni tatizo kwa jinsia zote.
5 comments:
Kwenye hasira people say things they dont mean....., na mwenza sababu huwa ameumia na yeye anataka amuumize mwenzake atasema chochote cha kumuuzi mwenzie, na kutoa hayo maneno mtu ndio anavyotoa steam.... ingawa matusi si vizuri lakini wanasema ni bora kitu ukakitoa kuliko kukiacha rohoni, sababu siku kikifumuka..., thats when unasekia fulani amengatwa sikio.... therefore sometimes arguments are healthy...
ni kweli kabisa...., tatizo ni pale ambapo hayo maneno yanaporudiwa rudiwa kila mkigombana mwenzio anakuita ma###y# hapo ndio panapoleta utata!
Hizo ni tabia mbaya na mtu mstaarabu inapaswa asimwite hata adui yake hayo maneno..., alafu hii nimeona kwa kina dada wengi anaweza akaanzisha ugomvi mbele ya marafiki ya mme wake au hata akamfata bar na kulianzisha... Mi naona ustaarabu kama mmekosana basi muitane chumbani mbali ya watoto na huko mpeane maneno na arguments zenu mkimaliza basi mnakumbatiana na let bygones be bygones....
ki ukweli inaumiza na kupoteza mapenzi kama wanvyo sema, sio vizuri kabisa yapo maneno ya kuambizana na mtu akakuelewa kuliko kauli zisizo na busara, tena wengine hufikia kusema najuta kwa nini niikuoa ni bahati mbaya tu. kweli jamani?
ki ukweli inaumiza sana, nakukatisha tamaa ya kuendelea kumpenda u mpendae, wanaume waheshimuni wenza wenu, nawanawake waheshimuni wa ume wenu, ila maneno ya kashifa hayapendezi wakati wa ugomvi kwani hata mkipatana unakuwa unajisikia vibaya ww ulie kuwa unatoa kashifa.
Post a Comment