Promote your business for free grow your business for life you don't need to spend more money anywhere.

THIS BLOG IS SPONSORED BY AHADIWAY ,ADVANTAGES FOR JOINING AHADIWAY BOON CAREER (ABC) CHAPTER = Employment opportunities within and outside the country. , Job experience , Self -employment , Field stations, part time jobs and chances to be trained.

Tuesday, February 1, 2011

bongo kazi kweli kweli


KAZI KWELI: "DOWANS,KUKU ANAYEKIMBIA NA PANZI WAKE MDOMONI"
HUTOKEA, kuku akimdaka panzi mdomoni, basi, ukimwandama ukimpigia kelele. Kuku huyo atakimbia na panzi wake mdomoni . Mara ile atakapoona umesitisha kumfukuza , na kelele pia. Basi, kuku huyo, taratibu ataanza kumla panzi wake.
Lakini, kama utaendelea kumwandama na kumpigia kelele, hutokea, kwa kuku anayekimbia na panzi mdomoni, kumtema panzi ili kuandamwa huko kwishe.

Dowans ni kama kuku na panzi wake mdomoni. Alishamdaka, kabla hajaanza kumla, Watanzania tumeamka na kuanza kumwandama Dowans huku tukimpigia kelele.
Kuku Dowans ameonyesha dalili za kuweweseka. Tukiongeza kupiga kelele, basi, upo uwezekano wa Dowans kumtema panzi.

Naam. Tuendelee tu kupiga kelele za ’ HATULIPI!, HATULIPI! ’- NON SI PAGA! Kwa Kiitalia. Yumkini panzi aliyemdomoni mwa Dowans anaweza kutemwa! Itakuwa nafuu kwetu

No comments:

Umesoma hizi hapa