Kumbe shanga ni zaidi ya urembo!
Rafiki yangu wa Kighana alitoa maelezo ambayo nadhani yalikamilika japo hakugusua umuhimu wake kwenye ngono….aliniambia kuwa huko kwao Shanga ni muhimu kuonyesha kuwa wewe ni mwanamke wa shoka au uliyekamilika. Ikiwa mwanamke huvai Shanga basi unaonekana hufai na hakuna mwanaume atataka kutoka na wewe/kuchumbia only kwa vile huna shanga kiuoni……hivyo wanawake wote wa Kighana wanavaa shanga no matter how beautiful, educated au westnized they are.
Turudi Nyumbani……nakumbuka niliwahi kumuuliza mama yangu (wao wanavaa shanga) faida ya shanga na yeye akanijibu kuwa ni kama sehemu ya “romance”….nikauliza ni sawa sawa na kubusu au kushikana? Akajibu “ndio”…..nikauliza inawezekanaje mtu asisimke kutokana na kuziona shanga tu au kuzishika-shika tu? Akanijibu kuwa “mwanaume anapozichezea humpa mwanake mtekenyo furani ambao hufamfanya ajisikie raha na hamu ya kungonoka (nyege) huanza kumpanda”.
Mimi kama Dinah nikahisi kuwa mwanaume anaetegemea kuchezea shanga ili mwanamke “anyegeke” atakuwa hana utundu wa kutosha wa kutumia mikono na vidole vyake ktk kuuchezea mwili wa mwanamke hasa ukizingatia kuwa mwanamke “hanyegeki” kwakuchezewa na vidole kiunoni tu bali kona nyingi ktk mwili wake Uvaaji wa shanga kiunoni ni moja kati ya tamaduni zetu waafrika, nakumbuka katika jamii ya Wanyamwezi (nadhani na Wasukuma pia as far as I remember miaka hiyo niliyoishi kona hizo za Tz ) shanga zilikuwa zikivishwa mtoto wa kike kiunoni na yule wa kiume alivalishwa kijikamba/uzi mweusi ambao huwa na vipande vidogo viwili au vinne vya mti akiwa mdogo.
Sina hakika kwanini ilikuwa hivyo ila nakumbuka niliwahi kuambiwa kuwa vijiti vile ni kumlinda mtoto dhidi ya malaika wabaya (kama ilivyo kwa tamaduni nyingine kuwapaka watoto wanja ili watishe) na shanga ni kuonyesha kuwa mtoto ni wa kike.
Mtoto napofikia umri fulani vikorokoro hivyo huondolewa na binti huvalishwa tena pale anapokua (vunja ungo/balehe), kule kwetu kila rangi ya shanga huwa na maana yake nikiwa na maana kama binti ni Bikira anavaa rangi fulani, kama uliolewa ukaachika wavaa rangi fulani, kama umeolewa wavalishwa rangi husika, kama siku hiyo wataka kufanywa (unanyege) basi wamvalia mumeo rangi husika, ikiwa ni mjamzito pia unapaswa kutuma ujumbe kwa kumvalia mumeo rangi fulani (ilikuwa mwiko kungonoka na mtoto tumboni) kama uko hedhini basi utalazimika kuongezea rangi nyekundu juu ya ile uliyonayo.
Itasaidia kama watakuja na rangi inayoashiria kuwa mtu kaukwaa a.k.a ana ngoma a.k.a UKIMWI.....wewe unaonaje? Ilikuwa ni mwiko kuachia shanga hizo zionekane au zionwe na watu wengine ambao hauko karibu nao kama mzazi, mume, kungwi (shangazi au bibi) n.k. tofauti na sasa ambapo shanga huvaliwa kama mtindo na huning’inizwa hovyo bila kujali maana au ujumbe unaotumwa na rangi za shanga wazivaazo.
Ni wazi kuwa wanawake hawa wanaojivalia shanga hizo na kuzionyesha hovyo huwapa wakati mgumu watu au jamii ambayo inathamini nakutunza utamaduni halisi wa mwanamke kutilia shanga kiunoni na maana ya rangi husika. Baadhi ya watu huwadhania wanawake wanaovaa shanga ovyo ni wapenda mambo ya ngono……hivi kuna mtu hapendi ngono hapa Duniani? Bila ngono si dhani kama mimi na wewe tungekuwepo, ngono ni muhimu ktk maisha ya mwanadamu…..au jina lake ndio linawatisha watu?
Haya basi tuseme kukutanisha na kuingiza uume ukeni…..bado halijakaa vema….kufanya mapenzi….aaah kufurahia utukufu na uumbaji wake mwenyezi Mungu. Swala muhimu hapo sio kuwashutumu na kuwahukumu wavaaji hao wa shanga bali ni kuwaeleza kwa uwazi swala zima la shanga……tuache utamaduni wa kubana-bana yale tuyajuayo ili sote tubaki kwenye mstari na ikiwa moja kati yetu atatoka mstarini at least atakuwa anajua nini anafanya au niseme ujumbe gani anaufikisha kwa watamzamaji wa shanga hizo.
Hii yote inatokana na wakuwa (bibi, shangazi, mama) ktk jamii kujisahau na kung’ang’ania mijini na kushindwa kuwatambulisha watoto wao tamaduni za huko watokako (asili yao) hivyo wanakuwa hawajui au wanajifanya “wazungu” na kutofuata tamaduni na badala yake wanafanya watakavyo…..
Mimi nimezaliwa Jijini Dar ila kule kwetu (asili yangu) wanavaa shanga na ninajua mambo mengi kuhusu tamaduni ya kwetu ikiwa ni pamoja na kutambulishwa maana halisi ya shanga na rangi zake……lakini mimi kama mimi sivai shanga sio tu kutokana na mtindo wangu wa mavazi bali pia sivutiwi au sijisikii vema ikiwa nitavaa shanga au hata nikiziona (hasa lundo) zinaning’inia kwa mtu mwingine (kama hiyo picha hapo juu) huwa naona ka’ uchafu vile….kama ni kijiuzi kimoja cha shanga au cheni poa ili kuongezea/ziba "kizugaji" uwazi fulani wa vazi lako if u know what I mean. *Wewe mwanaume kwanini unapenda mpenzi avae shanga kiunoni? Unazitumia vipi zikiwa kiunoni na zinakufanya ujisikie vipi? *Na wewe mwanamke ikiwa unavaa shanga mpenzi wako huzitumia vipi wakati wa kufanya mapenzi? Kumbuka hapa sote tunajifunza hivyo maelezo yako ya uwazi yatasaidia sana watu wengine hasa wale wasiojua utamaduni wa shanga na maana yake halisi.
Katika pitapita zangu mtandaoni nimekutana na mada hii (waweza kubofya HAPA kuisoma zaidi) ambayo inashabihiana na mada niliyoiweka hapa kwangu mwanzoni kabisa wakati naanza kublog, waweza kubofya HAPA kujikumbusha, ambapo ilikuwa ni changamoto kwa wanaume.
Katika pitapita zangu mtandaoni nimekutana na mada hii (waweza kubofya HAPA kuisoma zaidi) ambayo inashabihiana na mada niliyoiweka hapa kwangu mwanzoni kabisa wakati naanza kublog, waweza kubofya HAPA kujikumbusha, ambapo ilikuwa ni changamoto kwa wanaume.
No comments:
Post a Comment